Mikono Saidizi Ulimwenguni Kote
Kutana na Ami kutoka Japani
Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.
Yote kuhusu Ami
Lugha: Kijapani
Umri: miaka 10
Malengo na Ndoto: 1) Kuwa msanii (katuni za wanyama). 2) Kufanya mazoezi ya mchezo wa besiboli. 3) Kusoma mlango mmoja wa Kitabu cha Mormoni kila siku.
Familia: Mama, Baba, kaka watatu na dada mmoja
Mikono Saidizi ya Ami
Anaishi Okinawa, Japani. Kwa sababu ya UVIKO-19, wengi wa watu huko walipata taabu kupata chakula. Kwa hivyo kata ya Ami walifanya mpango wa kusambaza chakula. Yeye hakika alitaka kusaidia.
Wote walikutana katika jengo la Kanisa. Walichukuwa tahadhari wakati wakifanya kazi. Ami alivaa barakoa.
Ami aliweka maboksi ya katoni pamoja. Maboksi hayo yalipokuwa yamejaa, aliyafunga ili yaweze kufungwa vizuri kwa utepe. Ami aliendelea kufikiria jinsi Yesu alivyowalisha watu kwa vipande vya mikate na samaki. Alifurahi kuweza kusaidia kutoa chakula kwa watu kama Yeye alivyofanya.
Mambo Ayapendayo Ami
Mahali: Uwanja wa mchezo wa besiboli
Hadithi kuhusu Yesu: Wakati alipozaliwa
Wimbo wa Msingi: “I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3)
Chakula: Nyama
Rangi: Zumaridi ya kijani
Masomo shuleni: Maarifa ya Jamii na Mazoezi ya Viungo