2022
Kusaidia Kama Yesu
Januari/Februari 2022


Rafiki kwa Rafiki

Kusaidia Kama Yesu

Picha
girl pushing young boy in stroller

Nilipokuwa katika Msingi, kaka yangu alikuwa mtoto anayeanza kutembea, na dada yangu alikuwa mtoto mchanga. Mama yangu alikuwa na shughuli nyingi sana akiwashughulikia wao wakati wa mchana, hivyo nilipofika nyumbani kutoka shuleni, nilimsaidia. Nilimweka kaka yangu kwenye kiti cha kumtembezea na kuzunguka pamoja naye mtaani petu. Tulizungumza kuhusu uzuri wa ulimwengu na kuangalia ndege, wadudu, na wanyama wadogo wadogo wafugwao na majirani zetu. Kilikuwa kitu kidogo, lakini kilileta tofauti kubwa! Kilimsaidia mama yangu kujiona mwenye furaha na kupumzika. Kiliisaidia familia yote. Ilikuwa njia ya kusaidia kama Yesu anavyotaka sisi tusaidie.

Je, Wewe Unawezaje Kusaidia?

Picha
Jesus with children

Kama watoto wa Msingi, ninyi mnaweza kufanya tofauti kubwa kwa matendo yenu madogo ya ukarimu. Unapotumia mikono yako ya usaidizi kuwahudumia watu wengine, unamwakilisha Yesu Kristo. Unawasaidia watu wengine kuhisi upendo Wake.

Jifunze hadithi za Yesu. Halafu jiulize, “Je, Yesu angefanya nini?” Kuna watu kote kukuzunguka wewe ambao wanahitaji msaada. Baadhi yao wako nyumbani mwako, au pengine ng’ambo tu ya mtaa wako.

Unapofanya mambo yaliyo rahisi ya kusaidia, Roho Mtakatifu atakusaidia wewe ujisikie vizuri ndani yako. Utajua kwamba umefanya kile ambacho Yesu angekifanya.

Ni muhimu pia kukubali msaada kutoka kwa watu wengine. Tunaposaidiwa na watu wengine, tunaweza tukauhisi upendo wa Mwokozi kwetu sisi pia!

Ninawapenda! Ninajua kwamba Yesu Kristo anawapenda ninyi! Utausikia upendo Wake, unapotumia mikono yako ya usaidizi kuwahudumia wengine.

Mikono Yako ya Usaidizi

Yote kuhusu Wewe

Umri:

Kutoka kwa:

Lugha:

Familia:

Malengo na Mipango:

Tuambie kuhusu wakati wewe uliposaidia nyumbani au katika jumuiya yako:

Unajisikia vipi unapowasaidia watu wengine au kumfuata Yesu?

Mapendeleo Yako

Mahali:

Hadithi kuhusu Yesu:

Wimbo wa Msingi:

chakula:

Rangi:

Somo shuleni:

Chapisha