2022
Wewe ni Mtoto Mpenndwa wa Mungu
Januari/Februari 2022


Kutoka Urais wa Kwanza

Wewe ni Mtoto Mpendwa wa Mungu

Imechukuliwa kutoka kwenye Tangazo la Rafiki kwenda kwa Rafiki kwa ajili ya Watoto: 2021.

Picha
pictures of children’s faces

Wapendwa rafiki zangu wadogo, Ninawapenda ninyi! Ninapowaona ninyi, ninafikiria juu ya vitukuu wangu. Je, mlijua kwamba katika familia yangu, tunao vitukuu 100 chini ya umri wa miaka 12? Ni werevu na ni wa thamani sana, kama ninyi tu.

Wewe ni mtoto mpendwa wa Mungu Tafadhali kumbukeni hilo jambo. Kama kamwe hautasahau ukweli huo mmoja halisi, unaweza kukabliana na tatizo lo lote kwa imani na ujasiri.

Wakati unapobatizwa na kuthibitishwa, wewe unafanya ahadi kwamba utamfuata Bwana. Naye anakuahidi kwamba atamtuma Roho Wake ili akuongoze. Fikiria tu juu ya nuru na upendo unaoweza kuuleta ulimwenguni kama mfuasi mwaminifu wa Yesu Kristo!

Wapendwa marafiki zangu wadogo, ninajivunia sana kwa ajili ya kila mmoja wenu. Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anakulindeni ninyi. Yeye anawapenda ninyi sana, na mimi vivyo hivyo.

Mpango wa Furaha wa Baba wa Mbinguni

Picha
Page from the January/February 2022 Friend Magazine.

Paka rangi picha hizi ili kujifunza zaidi kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni. Soma zaidi katika Ibrahimu 3–5.

Niliishi na Baba wa Mbinguni kabla sijazaliwa.

Alimwagiza Yesu Kristo kuumba ulimwengu kwa ajili yetu sisi.

Yesu alitengeneza jua, mwezi, na nyota ili vitoe nuru.

Yesu alitengeneza dunia nzuri yenye miti na maua. Alitengeneza samaki, ndege, na wanyama.

Kisha Baba wa Mbinguni akawaweka Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza, juu ya dunia.

Baba wa Mbinguni ananipenda mimi na kunilinda.

Vielelezo na Elise Black

Chapisha