Siyo Mpweke Sana
Damián alitamani familia yake wangekuja wote pamoja kanisani.
Damián aliangalia katika begi lake la mgongoni ili kuona kama alikuwa na kila alichokihitaji. Nguo za kanisani? Sawa. Viatu? Sawa. Kitabu cha Mormoni? Sawa. Akafunga zipu ya begi lake la mgongoni, na kuliweka begani, na akaongoza mlangoni.
“Mama!” Damián aliita. “Ninakwenda kwa Abuela na Abuelo!”
Mama alikuwa anakunja taulo “Hakikisha unawasaidia bibi na babu yako.” Mama alisimama ili kumpa Damián kumbatio kubwa. “Najua unatamani kwenda kanisani pamoja nao. Muwe na wakati mzuri kesho.”
“Asante,” alisema Damián. Lakini natamani wewe ungekuja pamoja nami, yeye aliwaza.
Damián alitembea kuelekea kituo cha basi. Kila Jumamosi, alipanda basi kuvuka mji wake katika Ecuador na kwenda nyumbani kwa Abuela na Abuelo. Alikaa usiku huo pamoja nao. Kisha alikwenda kanisani pamoja nao siku iliyofuata.
Jumapili asubuhi, alivaa nguo zake tayari kwa ajili ya kanisa. Alifunga vifungo vya shati lake. Akavaa viatu vyake. Alitembea kwenda kanisani kanisani na Abuela na Abuelo.
Damián alilipenda kanisa. Alipenda kuimba nyimbo na kupokea sakramenti. Alipenda kuwaona marafiki zake pia. Lakini alitamani familia yake yote ingekuwa pamoja naye.
Mchana ule, Damián, Abuela, na Abuelo walitembea kwenda nyumbani kwa Kaka na Dada Ruiz. Walikuwa wakienda kufanya pamoja jioni ya nyumbani. Abuela alileta bakuli la matunda kwa ajili ya kitindamlo.
Somo lilikuwa kuhusu Yesu. Damián alipaka rangi picha ya Yesu akisikiliza lile somo. “Yesu anaelewa kila kitu tunachohisi,” Kaka Ruiz alisema. “Hata tunapohisi kuhuzunika.”
Damián aliiangalia ile picha yake ya Yesu. Ilimfanya ajisikie mwenye furaha kwamba Yesu anajua jinsi yeye alivyojisikia.
Baada ya sala ya kufunga, Abuela alisema, “Nimeleta matunda. Nani anataka?”
“Mimi?” Damián alisema. Kitindamlo kitamu cha malai, ndicho apendacho Damián! Na Abuela alioka vitobosha vizuri sana.
Baada ya jioni ya nyumbani, Abuela alitembea na Damián kwenda kituo cha basi ili aweze kwenda nyumbani. Damián aliangalia chini ardhini.
“Je, kuna kitu cho chote kibaya?” Abuela aliuliza.
Damián alikunja uso. “Ningetamani familia yangu yote ingekuja kanisani pamoja na sisi?
“Mimi pia,” Abuela alisema. Alimpa Damián kumbatio. “Lakini familia yako inakupenda sana. Na vivyo hivyo Abuelo na mimi na wengine wengi!”
Basi nalo lilisimama. Damián alikaa dirishani na akampungia mkono wa kwaheri kwa Abuela wakati basi lilipokuwa likiondoka.
Damián alifikiria kuhusu kile ambacho Abuela alikuwa amekisema. Yeye alifikiria kuhusu Mama na kaka yake na dada yake. Yeye alijua kuwa walimpenda sana. Kisha akawaza kuhusu mwalimu wake wa Msingi. Na familia ya Ruiz. Na Abuela na Abuelo. Hawa wote walimpenda pia.
Zaidi ya yote, Damián alijua kuwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimpenda. Na hilo lilimfanya hasijisikie kuwa mpweke tena.