Waanzilishi katika Kila Nchi
Dinis Anatafuta Jibu
Godoro la jozi za vitanda lilitoa kelele wakati Dinis akijigeuza. Amejitupa na kujigeuza usiku wote. Lakini hakuweza kulala tu.
Je, itakuwaje kama wamisionari hawakuwa sahihi? Dinis aliwaza. Je, itakuwaje kama kanisa siyo la kweli? Je, itakuwaje kama niko kwenye njia isiyo sahihi? Maswali yaliendelea kunisumbua.
Familia ilijiunga na Kanisa miaka miwili kabla, wakati alipokuwa na miaka 10. Wakati wamisionari walipowafundisha, Dinis alijisikia hivyo kwamba walichofundishwa kilikuwa cha kweli. Dinis na familia yake walikuwa baadhi ya watu wa kwanza kujiunga na Kanisa huko Ureno. Dinis alikuwa mwanzilishi!
Lakini hivi karibuni ameanza kujitilia mashaka. Je, itakuwaje kama kubatizwa halikuwa chaguo sahihi?
Dinis hakumwambia ye yote kama alikuwa na shaka. Siyo kaka zake, siyo dada zake. Wala wazazi wake. Lakini usiku wa leo, ndicho kitu pekee alichoweza kukiwaza.
Dinis alivuta pumzi. Aliangalia chini kwenye kingo ya kitanda. Kaka zake walilala fo fo fo kwenye kitanda cha chini yake. Dinis alikuwa peke yake.
Alijua alihitajika kumwomba Mungu ili kujua kama Kanisa ni la kweli. Alipiga magoti katikati ya kitanda chake. Akainamisha kichwa chake na kuanza kusali.
“Tafadhali, Mungu,” Dinis alisema kwa sauti ndogo. “Naomba nijue kama kweli Joseph Smith alikuona wewe na Yesu.”
Dinis alikuwa ameomba mara nyingi kabla ya hii. Lakini safari hii ilikuwa tofauti. Dinis hakika alitaka kujua. Alisali kwa bidii zaidi ili apate msaada kuliko alivyowahi.
“Sitaki kukosea,” alinong’ona. “Ninahitaji tu kujua kile kilicho sahihi.”
Kisha Dinis alihisi kitu fulani. Hisia ilikuwa yenye nguvu na tulivu. Ilikua hadi ikatawala mwili wake wote. Alihisi kama angepasuka kwa kujawa na shangwe!
Dinis alijua kuwa hisia hiyo ilikuwa ni Roho Mtakatifu. Mungu alikuwa amejibu sala yake! Wamisionari walikuwa sahihi. Joseph Smith hakika alikuwa nabii. Na kwa kubatizwa halikuwa tu chaguo zuri. Lilikuwa chaguo bora zaidi.
Dinis alilala chali na kutazama darini. Mashaka yake yakapotea. Alilivuta blanketi lake kujifunika. Kabla hajajua, alikuwa usingizini.
Kadiri Dinis alivyoendelea kukua, daima alikumbuka usiku ule wakati aliposali kwenye jozi yake ya kitanda. Alijua kuwa alikuwa kwenye njia sahihi kama muumini wa Kanisa la Yesu Kristo. Na alijua kwamba Baba wa Mbinguni daima angesikia sala zake.