2022
Yesu Aliwasaidia Watu wenye Uhitaji
Januari/Februari 2022


Kusaidia Kama Yesu

Yesu Aliwasaidia Watu wenye Uhitaji

Picha
Jesus helping up a sick man

Alipokuwa duniani, Yesu aliwaponya watu walio kuwa wagonjwa. Aliwalisha wale waliokuwa na njaa. Aliwafariji watu waliojisikia kuwa wapweke.

Yesu pia aliwafundisha wanafunzi Wake kuwasaidia wengine. Alisema wanapaswa kuwapa chakula, maji, na mavazi wale waliohitaji. Aliwaambia wawatembelee watu waliokuwa wapweke. Yesu alisema kwamba wakati wakiwatumikia wengine, ni kama wanamtumikia Yeye.

Picha
boy carrying firewood

Familia yangu inamtumikia Dada Rosa. Dada Rosa ana umri wa miaka 90, hivyo hawezi kutoka nje ya nyumba yake. Ninamsaidia Baba kupakia na kusafirisha kuni kwa ajili ya Rosa.

Ignacio G., umri miaka 9, Canelones Department, Uruguai.

Chapisha