2022
Shajara za Baba
Januari/Februari 2022


Shajara za Baba

Hadithi hii ilitokea huko Tahiti.

Picha
boy sitting on bench, reading

Allan alikaa kwenye bechi nje ya nyumba yao. Jua lilikuwa linazama. Matawi ya michikichi ilisimama dhidi ya anga la rangi ya pinki na chungwa.

Aligeuza ukurasa wa kile kitabu alichokuwa anakisoma. Hakikuwa na picha zo zote. Lakini Allan hakujali. Alipenda kukisoma kitabu hiki.

Macho yake yalipitia haraka haraka juu ya mwandiko mzuri wa Babaye. Alikumbuka sehemu hii! Daima ilimfanya acheke.

Hapo hapo, Baba akatoka nje. “Je, nini kinakuchekesha?”

“Ninasoma moja ya vitabu vyako.” Allan alitabasamu. “Ninapenda sehemu inayohusu nazi.

“Oh, unamaanisha shajara zangu.” Baba akakaa pembeni ya Allan. “Zinaelezea hadithi za maisha yangu. Lakini siyo tu kuhusu mimi. Wewe uko humo pia. Na pia Mama, na kaka na dada zako.

“Kama vile Nefi!” Allan alisema. “Yeye aliandika hadithi kuhusu maisha yake, na aliandika kuhusu familia yake pia.”

“Sawa!” Baba alisema.

“Ninapenda sehemu zinazokuhusu wewe zaidi,” Allan alisema. “Kama wakati ulipokuwa mmisionari hapa Tahiti.”

“Ninapenda hadithi kukuhusu wewe zaidi,” Baba alisema. “Je, ulijua kuwa tulikuita wewe kwa jina la katikati la Mzee Bednar?”

“Hamkuwahi kuniambia hilo! Siwezi kungoja kusoma sehemu hiyo.”

Baba alitabasamu. “Kuna hadithi nyingi katika shajara zangu. Nimekuwa nikiandika katika shajara tangu nikiwa na miaka minane.”

Picha
boy reading journal with his dad

“Tangu ukiwa na miaka minane?” Allan aliuliza. “Huo hakika, hakika ni muda mrefu sana.”

Baba alicheka. “Mimi siyo mzee sana.”

Allan alifikiri kwa dakika chache. “Mimi nafikisha miaka minane hivi karibuni” alisema. “Je, naweza kupata shajara kama zawadi yangu ya siku ya kuzaliwa?”

“Bila shaka!” Baba alisema.

“Kisha nitaanza kuandika hadithi zangu ili siku moja watoto wangu waweze kuzisoma.”

“Unaonekana kama utamaduni mzuri kwa familia!” Baba alisema.

Chapisha