Kumfuata Yesu kwa Pamoja
Msingi huko Denbighshire, Wales, walitengeneza picha hii ya Ono la Kwanza kwa pamoja!
Ninasoma maandiko yangu kila siku ili kujifunza kitu kipya. Ninatarajia kwenda kuhudumu misheni!
Rashad E., umri miaka 10, West Virginia, Marekani
Ninao wasiwasi. Mama yangu alinipa baadhi ya mawazo ambayo yaliufanya upungue, lakini haujatoweka. Niliomba kwa ajili ya msaada, na wasi wasi wangu ukaanza kupotea!
Felix G., umri miaka 10, California, Marekani
Nililiremba boksi na nikalijaza chupa za maji na vipasha joto mikono kwa ajili ya watu waleta vitu ambao hutembelea jengo letu na makazi. Ninajaribu kuhudumu kama Yesu!
Ellie Rose M., umri miaka 6, New York, Marekani
Tulikuwa tukijifunza kuhusu Saskatchewani huko shuleni. Niliweza kuwaeleza wana darasa wenzangu na mwalimu kwamba dada yangu anahudumu kama mmisionari huko!
Jacob S., umri miaka 7, Alberta, Kanada
Tulitengeneza maboti! Moja lilikuwa boti la mababu zetu lililotia nanga wakati walipohamia Marekani kutoka Swideni vizazi sita vilivyopita.
Aksel na Declan M., umri miaka 6 na 9, North Carolina, Marekani
Nilisikia maneno mabaya, ambayo yalinifanya nikose faraja. Mara nilipokuwa nyumbani, nilisali ili nipate msaada niweze kuyasahau yale maneno. Baba wa Mbinguni alijibu maombi yangu.
Emree H., umri miaka 10, Oregon, Marekani
Mmoja wa wana darasa wenzangu alikuwa anaogopa kuhusu kwenda shuleni. Nilifika shuleni mapema kila siku ili nimsubiri yeye ili asijione yuko pekee yake. Kuwasaidia wengine kunanifanya nijisikie vizuri kwa sababu ninamfuata Yesu.
Fang Z., umri miaka 6, Hsinchu, Taiwani
Emmy S., umri miaka 8, Michigan, Marekani
Madeline H., umri miaka 9, Ulaanbaatar, Mongolia
“Familia yangu,” Janus C., umri miaka 7, New South Wales, Australia