2022
Carolina Anawajali Wengine
Januari/Februari 2022


Carolina Anawajali Wengine

Je, Carolina angewezaje kumsaidia rafiki yake?

Picha
girl playing hopscotch with boy who is bald

Carolina alijaribu kumsikiliza mwalimu wake. Lakini hakuweza kuacha kumtazama rafiki yake Ramón. Hakuwa na nywele yo yote!

Nywele zake zimekuwa zikimtoka kwa kipindi sasa. Sasa alikuwa na kipara.

Carolina alisikia sauti nyuma yake. Cesar na Luis walikuwa wakicheka kwa sauti ya chini chini. Yeye alitumaini hawakuwa wakimcheka Ramón.

Asubuhi yote, Ramón alipindisha mabega yake. Hakunyosha mkono wake. Alionekana kuwa mwenye huzuni. Carolina alitamani angeweza kumsaidia kujisikia vizuri zaidi.

Hatimaye ukaja muda wa kucheza nje. Ramón alikuwa wa kwanza kutoka nje ya darasa. Carolina alipotoka nje, hakuweza kumwona po pote! Hakuwa akicheza mpira wa miguu. Hakuwa akipanda juu ya nguzo. Na hakuwa anacheza hopscochi na mwalimu.

Yuko kule! Ramón alikuwa amesimama kwenye kona ya uwanja. Na Cesar na Luis wako huko pia. Carolina alitembea kuwasogelea.

“Angalia jinsi kichwa chake kilivyo kikubwa!” Cesar alipiga kelele.

Luis alicheka. “Hata mimi ningenyoa kichwa changu pia kama ningekuwa na nywele mbaya kama hivi.”

Ramón aliikunja mikono yake ngumi. Alionekana kama anataka kulia.

Carolina akamkimbilia Ramón. “Je, unataka kucheza na mimi?” alimwuliza. Akanyosha mikono yake, na wakaondoka pamoja. Waliendelea kutembea hadi walipomkaribia mwalimu. Hakuna ambaye angewasumbua hapo.

“Je, unapenda kucheza hopskochi?” Carolina aliuliza.

Ramón alikubali kwa kutikisa kichwa. Akachora mistari kwa chaki ardhini.

“Je, uko sawa?” aliuliza.

“Niko sawa sasa.” Ramón akatabasamu. “Asante kwa kunisaidia.”

Carolina alitabasamu. Alifurahi kuwa jasiri vya kutosha kumsaidia rafiki yake.

Chapisha