Salamu kutoka Ivory Coast!
Ungana na Margo na Paolo wanaposafiri ulimwenguni ili kujifunza kuhusu watoto wa Mungu.
Ivory Coast, au Côte d’Ivoire, ni nchi iliyopo Afrika Magharibi.
Ina Waumini 52,000 na Inakua
Mzee D. Todd Christofferson alitembelea waumini wa huko mwaka 2019.
Habari!
Lugha rasmi ni Kifaransa. Zaidi ya lugha 70 huzungumzwa hapa pia.
Muda wa Chakula cha Jioni
Chakula maarufu ni yassa. Inatengenezwa na kuku au samaki na vitunguu, limao, haradali na pilipili kali.
Sanaa na Muziki
Watu wa Ivory Coast wana staili nyingi za sanaa na muziki. Je, unapenda kuunda nini?
Hekalu Lipo Njiani
Hekalu linajengwa katika jiji kubwa zaidi la Ivory Coast, Abidjan. Watoto hawa walisaidia kuchimba msingi kwa ajili ya hekalu jipya.