2022
Tom na Mafua Makali
Mei/Juni 2022


Waasisi katika Kila Nchi

Tom na Mafua Makali

Tom alijua Mungu angewasaidia.

Picha
boy helping sick dad drink

“Haya hii hapa, Tamā (baba),” Tom alisema kwa upole. Baba yake Tom polepole aliketi kwenye mkeka wake wa kulalia. Tom alimsaidia kunywa sharobati safi ya nazi.

Tama na wengine wa familia ya Tom walikuwa wagonjwa kwa siku nyingi. Karibu watu wengine wote katika kijiji hicho walikuwa wagonjwa pia. Ugonjwa wa homa ya mafua ya Kihispania ulikuwa umekuja kwenye kisiwa hicho.

Tom akatoka nje. Alikuwa mmoja wa watu pekee waliokuwa na uwezo wa kuwatunza wengine. Na familia nyingi zilihitaji msaada.

Nahitaji sharobati zaidi ya nazi, Tom alijiwazia. Akapanda juu ya mnazi mrefu. Alipofika juu, alichuma nazi na kuzitupa chini.

Picha
boy climbing up coconut tree

Alipokuwa akishuka, Tom aliwaza kuhusu watu katika kijiji chake. Ilitisha kuona wengi wao wakiwa wagonjwa.

Mwaka mmoja mapema, kaka mdogo wa Tom, Ailama, aliugua. Hilo lilikuwa la kutisha pia. Tom na familia yake walisali ili apone.

Kisha Tamā akaota ndoto maalum. Ndoto hiyo ilimwonyesha jinsi ya kumsaidia Ailama kupata nafuu—kwa kupiga gome la mti wa wiliwili ili kupata sharobati yake. Tom alimsaidia Tamā kumtunza Ailama, na wakampa sharobati kutoka kwenye mti huo. Na Ailama akapata nafuu!

Tom alijua Mungu alikuwa amewasaidia wakati huo. Na alijua Mungu angewasaidia sasa.

Tom alizivunja nazi. Harufu nzuri ya sharobati ya nazi ilimfanya ahisi vizuri kidogo. Alitembea hadi nyumba ya pili kijijini hapo ili kuwagawia majirani zake sharobati. Kisha akaenda kwenye nyumba iliyofuata. Na iliyofuatia.

Wiki zilipita. Kila siku Tom alifanya kazi kwa bidii ili kumtunza kila mtu. Alikamata kuku ili atengeneze supu ya joto ili kuwapa watu. Alibeba ndoo za maji kutoka kwenye chemchemi kwa ajili ya watu kunywa.

Baadhi ya watu katika kijiji walikufa. Tamā alikufa pia. Ilikuwa ngumu sana kwa Tom. Kijiji kizima kilikuwa na huzuni. Lakini katika yote hayo, Tom alikumbuka kwamba Mungu alimpenda na angemsaidia.

Tom hakuacha kusaidia watu. Na baada ya muda, watu walianza kupata nafuu!

Hatimaye janga la homa liliisha. Watu waliacha kuugua. Tom na Ailama waliweza hata kwenda shuleni tena. Tom daima atamkumbuka Tamā. Lakini alijua siku moja angemuona baba yake tena. Na alijua kwamba Baba wa Mbinguni daima angekuwa pale kumsaidia.

Samoa ni kundi la visiwa katika Bahari ya Pasifiki.

Leo kuna hekalu moja huko Samoa.

Nyumba ya kitamaduni huko Samoa iitwayo fale, haina kuta.

Janga la homa ya mafua ya Kihispania lilifika Samoa mnamo 1918.

Tom alikuwa na umri wa miaka 12 wakati janga hilo lilipoanza.

Kijiji cha Tom, Sauniatu, kilijengwa na kundi la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Picha
PDF of story

Vielelezo na Corey Egbert

Chapisha