2022
Ruthu na Naomi
Mei/Juni 2022


Hadithi za Maandiko

Ruthu na Naomi

Picha
Old Testament couple getting married

Naomi na familia yake walikwenda kwenye nchi mpya kwa sababu ya njaa. Walikutana na msichana anayeitwa Ruthu. Ruthu aliolewa na mwana wa Naomi.

Picha
man laying sick in bed

Kisha mume wa Ruthu alifariki. Ruthu alikuwa na huzuni sana.

Picha
older woman in blue scarf, looking sad

Naomi naye alihuzunika sana. Naomi aliamua kurejea katika nchi aliyotoka.

Picha
Ruth and Naomi talking with sunset behind them

Naomi akamwambia Ruthu arejee kwa familia yake. Lakini Ruthu alimpenda Naomi. Aliahidi kuambatana na Naomi na kumtunza.

Picha
Ruth gathering basket of grain

Ruthu na Naomi walikuwa maskini. Kwa hiyo Ruthu alijitahidi sana kuwatafutia chakula.

Picha
Boaz talking to Ruth in a wheat field

Siku moja mwanaume anayeitwa Boazi alimwona Ruthu akikusanya mabaki ya nafaka katika shamba lake moja.

Picha
Boaz talking to man in field

Boazi alikuwa mwema. Aliwaambia wafanyakazi wake wamuachie Ruthu chakula cha ziada.

Picha
Ruth, Boaz, and Naomi looking at new baby

Baadaye Ruthu na Boazi walioana. Walipata mtoto wa kiume. Naomi alimsaidia kumtunza.

Picha
girl helping serve dinner in backyard

Ninaweza kusaidia kuwatunza wengine. Ninaweza kuwa mkarimu kwa wale wanaohitaji.

Picha
coloring page of boy giving drink to grandpa

Vielelezo na Apryl Stott

Chapisha