Mikono ya Usaidizi Ulimwenguni Kote
Kutana na Animankutoka Ivory Coast
Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.
Yote kuhusu Animan
Umri: miaka 12
Lugha: Kifaransa
Malengo na ndoto: 1) Kujifunza kuhusu nchi zingine na tamaduni. 2) Kutumikia misheni.
Familia: Baba, mama wa kambo, na ndugu watano
Mikono Saidizi ya Animan
Animan husaidia kwa kujaza pipa la maji ambalo familia yake hutumia kwa ajili ya kuoshea vitu. Yeye pia husaidia familia yake katika duka lao. Anafagia, kusafisha na kujaza rafu. Yeye ni mwaminifu kwa wateja.
Animan daima hujaribu kuwa mfano mzuri. Wakati mwingine watu humdhihaki kwa kutokunywa pombe. Lakini wengine humuunga mkono anapotetea kile kilicho sahihi. Anasema kufanya kile kilicho sahihi humfanya ahisi kama ameshinda kombe! Animan ni shemasi. Anapenda kupitisha sakramenti kwa sababu inawasaidia watu kumkumbuka Yesu.
Vitu Pendwa vya Animan
Hadithi kuhusu Yesu: Wakati akisali katika bustani ya Gethsemane
“Children All Over the World” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 16–17)
Chakula: Foutou (mihogo iliyopondwa na ndizi)
Somo shuleni: Kifaransa