Timu na Vipaji
Timu bora hufanya kazi kwa pamoja na kusaidiana kila mmoja kuwa bora.
“Kimbia, Jillian, kimbia!” Baba alipiga kelele. Baba yake Jillian alikuwa ni kocha wa timu ya mpira wa miguu ya Jillian. Walikuwa wakifanya mazoezi ya ziada kujiandaa na mchezo wa ubingwa. Jua lilikuwa kali, lakini Jillian aliendelea kukimbia.
Hatimaye baba akapiga filimbi. “SAWA, acha tupumzike.”
Jillian alichukua chupa yake ya maji na kukaa kwenye benchi pamoja na wavulana. Alikuwa msichana pekee kwenye timu, lakini hakujali. Wote walifanya kazi pamoja na kusaidiana kuwa bora. Ingawa alikuwa amechoka na ana jasho, alihisi furaha kucheza na timu yake.
“Baba, tumefanyaje leo?” Aliuliza.
Baba akatabasamu. “Vizuri! Nafikiri timu ipo tayari kwa mchezo.”
Jillian akatabasamu pia. Kazi yao yote ngumu ilistahili!
Akiwa njiani kuelekea nyumbani kutoka mazoezini, Jillian alimwona rafiki yake Mei. Walikuwa katika darasa moja la Msingi. Lakini Mei hakuwa amehudhuria Msingi kwa muda.
Jillian alitabasamu kwa Mei. “Mambo, Mei! Sijakuona kitambo darasa la Msingi. Mko Salama?”
Mei alitazama chini kwenye viatu vyake. “Mama yangu hapendi kwenda kanisani.”
“Kivipi?”
“Sijui.” Mei aliinua kichwa chake. “Inabidi niendelee na safari.”
Jillian alipunga mkono na kumtazama Mei akiondoka. Ninawezaje kumsaidia Mei? alijiuliza.
Jillian alipofika nyumbani, alicheza baadhi ya nyimbo za Msingi kwenye ukulele yake. Kisha akawaalika kaka zake waimbe pamoja naye. Waliimba hadi Mama akawaita kwa ajili ya chakula cha jioni.
“Nitamtembelea Dada Aurea kesho,” Mama alisema.
“Dada Aurea ni mama yake Mei, sivyo?” Jillian aliuliza. “Je, ninaweza kwenda nawe? Mei amekuwa haudhurii darasa la Msingi. Na nilipomwona leo, alionekana kuwa na huzuni.”
“Hakika, unaweza kuja,” Mama alisema.
“Nitaleta ukulele yangu! Ninaweza kucheza nyimbo za Msingi. Ninaamini kwamba anatamani kuziimba,” alisema Jillian.
Walipofika nyumbani kwa Mei siku iliyofuata, Jillian alimpa Mei kumbatio kubwa. Wakati mama zao wakiongea, wasichana walienda nje. Jillian alicheza ukulele yake, na Mei akachagua nyimbo. Walikuwa na furaha wakicheka na kuimba pamoja hadi wakati wa Jillian kuondoka ulipowadia.
“ilikuwa furaha kukuona leo,” Jillian alisema. “Tumekukumbuka kwenye darasa la Msingi.”
“Ndio, natamani ningekuja. Labda nitamuuliza tena mama yangu.”
Jumapili iliyofuata, Mei alikuwa kanisani. Jillian akaketi kando yake. “Nina furaha sana umeweza kuja,” alisema.
Mei alitabasamu. “Mimi pia.”
Siku chache baadaye ulikuwa wakati wa mchezo mkubwa wa mpira wa miguu. Jillian aliiomba timu kufanya maombi kabla ya mchezo. Kisha ilikuwa wakati wa kucheza. Jillian alikimbia kwa kasi alivyoweza. Alifanya kazi na timu yake kupata mpira na kufunga mabao. Timu yake ilishinda mchezo!
Usiku huo akiwa amelala kitandani, Jillian aliwaza kuhusu Mei na timu yake ya mpira wa miguu. Alifurahi kuwa sehemu ya timu, kama vile alivyofurahi kuwa sehemu ya Msingi. Wote walisaidiana. Jillian alifurahi kwamba angeweza kuwasaidia marafiki zake, iwe ni kanisani au uwanjani.