2021
Unganisha
Julai 2021


“Unganisha,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Julai 2021, ndani ya jalada la mbele.

Unganisha

Orin S.

17, British Columbia, Canada

Picha
mvulana

Picha na Christina Smith

Familia yangu ilifanya safari ya kupiga kasia ndani ya maji na hatukuona ardhi kwa zaidi ya wiki tatu. Baada ya wiki mbili, tulipigwa na dhoruba kali. Matanga yetu yakavunjwa na upepo, na mawimbi yaliipiga sitaha, na kuzamisha kabisa upande wa mbele wa boti. Juu ya hayo yote, tulikuwa karibia kuishiwa na maji ya kunywa—hivyo kama tungesalimika na dhoruba hiyo, bado tulikuwa na hilo la kuhofia.

Familia yangu ilisongamana kwenye sehemu pekee kavu ya boti hilo na kuomba kwa takribani saa moja. Sikujua kama tungelisalimika usiku huo, lakini nilijua kwamba, bila kujali lolote, ningelikuwa pamoja na familia yangu kwa sababu tulikuwa tumeunganishwa pamoja.

Tulipokuwa tumemaliza maombi, tuliona kwamba upepo ulikuwa umetulia na mawimbi yalikuwa yamekoma. Punde baadae, ikaanza kunyesha mvua, ambayo ni kwa nadra sana katika sehemu hiyo ya bahari. Tulitumia turubai kujaza matanki yetu na kimiujiza tulipata maji ya kutosha kumalizia safari yetu.

Tukio hilo lilinionyesha jinsi gani maombi yanaweza kuwa na nguvu na jinsi gani Baba wa Mbinguni anatujali. Ninapofikiria nyuma juu ya dhoruba ile, ninajua kuwa injili hii ni ya kweli na halisi.

Chapisha