2021
Ono
Julai 2021


“Ono,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 16–17.

Njoo, Unifuate

Ono

Mafundisho na Maagano 76

Picha
Ono

Baada ya kutafsiri Kitabu cha Mormoni, Bwana alimwamuru Joseph kupitia upya Biblia.

Alipoisoma Biblia Joseph alipata mwongozo wa kiungu kutoka kwa Bwana kufanya baadhi ya mabadiliko.

Joseph aliwaomba waandishi wamsaidie kuandika.

Kazi ilicheleweshwa wakati Bwana alipowaamuru Watakatifu kuhamia Ohio.

Baada ya kuhamia huko Ohio, Joseph alianza mapitio yake tena pamoja na Sydney Rigdon akisaidia kama mwandishi.

“Tunahitaji kuanza tena kazi yetu kwenye Biblia.”

Mnamo Februari 16, 1832, Joseph na Sidney walikuwa wakipitia kitabu cha Yohana katika Agano Jipya.

“… wale waliofanya mema, katika ufufuo wa wenye haki; na wale walifanya maovu, katika ufufuo wa wasio haki.”

“Hii inamaanisha nini?”

Ono kubwa likawafungukia.

Wakamwona Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni.

Pia wakajua kwamba kuna falme tatu huko mbinguni.

Wakaonyeshwa kwamba wale watakaorithi ufalme wa selestia watakuwa wa kwanza kufufuka.

“Hawa ndio wale ambao … wamekamilishwa kupitia kwa Yesu.”

Wakati ono hili lilipokwisha, wakastaajabu. Sydney alikuwa amechoka.

“Sidney hajazoea haya kama mimi nilivyo.”

Chapisha