“Kutimiza Ahadi Zetu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 32.
Neno la Mwisho
Kutimiza Ahadi Zetu
Kutoka kwenye hotuba ya mkutano mkuu wa Oktoba 2019.
Jioni moja katika ujana wangu, mama yangu aliketi pamoja nami kwenye mguu wa kitanda chake na kuzungumza kwa unyenyekevu kuhusu umuhimu wa kuishi Neno la Hekima. Aliniangalia moja kwa moja machoni mwangu, na nilihisi maneno yake yakipenya moyoni mwangu: “Niahidi, Ronnie, leo, kwamba daima utaishi Neno la Hekima.” Kwa dhati nilifanya ahadi hiyo kwake, na nimeishikilia kwa miaka hii yote.
Pia nilifanya uamuzi mapema wa kufuata sheria za Mungu, na kamwe sikuhitaji kufikiria upya juu ya hilo. Bwana amesema, “Mimi, Bwana, ninafungwa wakati ninyi mnapofanya ninayosema; lakini msipofanya ninayosema, ninyi hamna ahadi.” (Mafundisho na Maagano 82:10).
Kama Mtume wa Bwana Yesu Kristo, ninakualikeni ninyi kuzingatia ahadi na maagano mliyofanya na Bwana, na watu wengine kwa uadilifu mkubwa, mkijua kwamba neno lako ni dhamana yako. Ninakuahidini, mfanyapo hivi, Bwana ataimarisha maneno yenu na kukubali matendo yenu kadiri mnavyojitahidi kwa bidii bila kuchoka kujenga maisha yenu, familia zenu, na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Yeye atakuwa pamoja na ninyi, nanyi mnaweza, kwa kujiamini, kutarajia “kupokelewa mbinguni, kwamba huko [ninyi] mpate kukaa pamoja na Mungu katika hali ya furaha isiyo na mwisho” (Mosia 2:41).