2021
Unaweza!
Julai 2021


“Unaweza!” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 24–26.

Njoo, Unifuate

Unaweza !

Tunahitaji kukumbuka yale yote ambayo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wamefanya—na yale wanayoendelea kufanya—ili kutusaidia sisi kurithi ufalme wa selestia.

Mafundisho na Maagano 76

msichana

“Mimi? Katika ufalme wa selestia? Sidhani kama nitafika.”

Je, umewahi kuwa na fikra kama hiyo? Ndiyo, ni kawaida kujiuliza kama ni wema vya kutosha hususan inapoonekana kama tuko mbali sana na kuwa wakamilifu. Nyakati zingine unajisikia kama ufalme wa selestia haufikiki!

Lakini usikate tamaa. Madhumuni ya mpango wa Baba wa Mbinguni ni kukusaidia wewe kuwa kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kuishi pamoja Nao katika ufalme wa selestia. Na wewe uko katika nafasi nzuri zaidi kuliko unavyofikiria. Rais M. Russell Ballard, Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, ametukumbusha kwamba kuishi pamoja Nao tena “ni zaidi ya lengo letu—pia ni lengo Lao.”1

Zaidi ya kitu chochote, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanataka sisi sote tuishi katika ufalme wa selestia pamoja na Wao na familia zetu. Habari njema ni kwamba hatuhitaji kufika huko sisi wenyewe tu. Tunapokuja kwa Kristo na kumfuata Yeye, tunapokea nguvu na msaada tunaohitaji. Kwa sababu ya Upatanisho Wake, kurithi ufalme wa selestia siyo tu inawezekana, bali inafaa pia.

Hivyo, kwa msaada Wake, wewe unaweza kufanya hili! Unaweza!

Mpango wa Mungu ni kwa ajili ya Kila Mmoja

Ili kuingia ufalme wa selestia, tunahitaji kuwa na imani katika Yesu Kristo na kutafuta kuongeza hiyo imani. Tunahitaji kujitahidi kubadilika na kutubu kila siku. Tunahitaji kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu—na daima kumkumbuka Yesu Kristo na kufanya upya maagano yetu. Tunahitaji kuvumilia hadi mwisho. Kama haya ndiyo mambo unayotamani na unajitahidi kuyafanya, uko katika njia yako ya kuwa mmoja wa wale watakaorithi ufalme wa selestia.

Kwa kuongezea, Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, amefundisha kwamba wale wenye kustahili daraja la juu kabisa la ufalme wa selestia ni “wale ambao wamekidhi vigezo vya juu vya ufalme huu, ikijumuisha uaminifu kwenye maagano yaliyofanywa katika hekalu la Mungu na ndoa ya milele.”2 (Unaweza kujifunza zaidi kuhusu hili kwa kusoma Mafundisho na Maagano 76:50–7092–96).

Kama hili linakufanya wewe ujiulize maswali—au kuhofia—kuhusu matayarisho yako ya kuurithi ufalme wa selestia, kumbuka kwamba hiyo ni safari. Kila siku tunayochagua kuwa zaidi kama Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo ni siku ambayo tunasogea karibu zaidi na kuwa mtu wa kiselestia zaidi—na karibu zaidi na ufalme wa selestia. Ndiyo, kutakuwa na kujikwaa, makosa na dhambi kwetu sisi sote. Kumtegemea Yesu Kristo tunapotubu kila siku ndiyo swala la muhimu. Safari hii ni ya kutumainiwa kwa sababu ya yale yote ambayo Yeye na Baba yetu wa Mbinguni wamefanya—na kile ambacho Wao wanaendelea kufanya—ili kutusaidia sisi kufika huko.

Tunaye Mwokozi

Yesu Kristo

Mwokozi anatoa njia kwa ajili yetu sisi kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni. Joseph Smith aliwaelezea wale wanaoishi katika ufalme wa selestia kama walio “upokea ushuhuda wa Yesu” na walio “kamilishwa kwa njia ya Yesu … aliyekamilisha upatanisho huu mkamilifu kwa njia ya umwagikaji wa damu yake Yeye mwenyewe” (Mafundisho na Maagano 76:51, 69).

Kuwa wakamilifu katika Yesu Kristo hakumaanishi kwamba hatufanyi makosa kamwe. Inamaanisha kwamba tunatubu na kujaribu kuwa bora kila siku, tukimtegemea Mwokozi na nguvu ya Upatanisho Wake ili kutusaidia kubadilika. Tufanyapo hivi, neema Yake inaturuhusu sisi kusonga kuelekea daraja lile la juu zaidi la ufalme wa selestia ambako tutaishi pamoja na Yeye, Baba wa Mbinguni, na familia zetu milele. Pia tutapokea vyote ambayo Baba Yetu wa Mbinguni anavyo. Hakuna chochote katika hivi ambacho kingewezekana bila ya Mwokozi.

Tunalo Kanisa.

Rais Oaks alifundisha kwamba pia Kanisa liko hapa “ili kuwasaidia watoto wote wa Mungu kuelewa uwezekano wao wa kuwa na kupata hatima yao ya juu kabisa. Kanisa hili linaishi ili kutoa kwa wana na mabinti wa Mungu njia ya kuingia ndani ya na kuinuliwa katika ufalme wa selestia.”3 Hii hufanyika kupitia utiifu kwa ibada na maagano ya injili.

hekalu

Ibada na maagano haya yanahitaji ukuhani, ambao unapatikana tu katika Kanisa la kweli la Mungu. Katika njia hizi na nyinginezo, Bwana na Kanisa Lake wanatusaidia sisi katika safari yetu ya kuwa bora tuwezavyo ili mioyo yetu itayarishwe ili siku moja kurithi vyote ambavyo Baba wa Mbinguni anavyo na kupata uzima wa milele.

Endelea Kusonga, na Usikate Tamaa!

Safari hii kuelekea ufalme wa selestia ni ya matumaini, lakini daima siyo rahisi. Baba wa Mbinguni analijua hilo. Yeye na Yesu Kristo wameahidi kutusaidia na kutuimarisha kila hatua njiani.

mawio

Picha kutoka Getty Images

Songa mbele, na usikate tamaa. Tutapata msaada kadiri tunavyojitahidi kumfuata Mwokozi, tuishi kama tunaostahili kupokea na kutendea kazi misukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu, na tutambue pale tunapoweza kuboresha. Tunapopita katika maisha kwa imani katika Yesu Kristo na kutubu pale tunapohitajika kufanya hivyo, Baba yetu wa Mbinguni atatusaidia kubadilika kuwa bora zaidi.

Kuwa mwenye kustahili ufalme wa selestia hakukamilishwi na tendo kuu moja. Ni matokeo ya kuendelea kuchagua kumfuata Mwokozi na kutegemea juu ya matumaini na hakikisho ambalo linakuja kutoka kwenye injili Yake.

Kwa hivyo, kama unajitahidi kumfuata Mwokozi na bado una hofu kama utafika kwenye ufalme wa selestia, ishara zote hutoa jibu la “Ndiyo! Utaweza!” Hili ndilo Baba wa Mbinguni analokusudia kwetu sisi sote. Na kama Rais Oaks alivyofundisha, yote haya yanawezekana “kwa sababu ya upendo wa Mungu kwa watoto wake na kwa sababu ya upatanisho na ufufuko wa Yesu Kristo, ‘ambaye anamtukuza Baba, na kuokoa kazi zote za mikono yake’ [Mafundisho na Maagano 76:43].”4

Muhtasari

  1. M. Russell Ballard, mkutano mkuu wa Apr. 2017 (Ensign au Liahona, Mei 2017, 65).

  2. Dallin H. Oaks, “Ukengeufu na Urejesho,” mkutano mkuu wa Apr. 1995 (Ensign, Mei 1995, 86).

  3. Dallin H. Oaks, “Ukengeufu na Urejesho” (87).

  4. Dallin H. Oaks, “Ukengeufu na Urejesho” (87), msisitizo umeongezwa.