2021
Sehemu ya Burudani
Julai 2021


“Sehemu ya Burudani,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 28–29.

Sehemu ya Burudani

Picha
Sehemu ya Burudani

Mzingile wa Wakati wa Karamu

Ndugu hawa watatu kila mmoja anahitaji kufika mjini ili kupeleka mialiko kwa ajili ya karamu ya kumbukizi ya miaka 90 ya kuzaliwa kwa bibi yao. Je, unaweza kuwasaidia kupata njia tatu kupitia mzingile huu ambazo zitawafikisha kwenye kila nyumba yenye paa jekundu, lakini bila ya yeyote kati ya ndugu wawili kutumia mtaa mmoja?

Fumbo la Rais Nelson

Ona ni vizuri kiasi gani wewe unaweza kufanya katika fumbo hili la kweli au si kweli kuhusu Rais Russell M. Nelson

Kweli au Si kweli?

  1. Ili kuwasaidia wazazi wake, ambao hawakuwa waumini hai wa Kanisa, kuishi Neno la Hekima, yeye alivunja kila chupa ya pombe ya wazazi wake na kuimimina pombe kwenye mfereji.

  2. Yeye alikuwa daktari mpasuaji wa ubongo.

  3. Alisaidia katika ugunduzi wa mashine ya moyo na mapafu.

  4. Rais Nelson alifanya upasuaji wa kwanza wa wazi wa moyo huko Utah.

  5. Anao wana tisa na binti mmoja.

  6. Ana utambuzi mzuri wa sauti

  7. Alifanya upasuaji wa moyo kwa Mzee Spencer W. Kimball, ambaye baadaye alikuja kuwa Rais wa Kanisa.

  8. Karibia azame majini wakati mmoja katika safari ya familia kwa chelezo.

  9. Daima alitaka kujifunza jinsi ya kuteleza kwenye theluji, lakini hakupata muda.

  10. Kutokana na kuibuka kwa vita, Rais Nelson hakuhudumu misheni.

Vichekesho

Picha
giza totoro isipokuwa macho ya katuni

Bado nasema ni mapema sana kwa kujifunza maandiko kama familia!

Kevin Beckstrom

Picha
mtu mwenye pajama aliyefunikwa kwa nguo na vitu vingine vya nyumbani, mwanamke kitandani akiwasha taa

Nilifikiri kulikuwa na tetemeko la ardhi au dubu ameingia ndani ya nyumba au kitu fulani! Kwa nini hukuwasha taa?

Sikutaka kumwamsha yeyote.

Val Chadwick Bagley

Majibu

Fumbo la Rais Nelson 1. Kweli; 2. Si kweli—yeye alikuwa daktari mpasuaji wa moyo; 3. Kweli; 4 Kweli; 5 Si kweli—ni mabinti tisa na mvulana mmoja! 6. Kweli; 7. Kweli; 8. Kweli; 9. Si kweli—yeye amekuwa mtelezaji kwenye theluji maisha yake yote; 10. Kweli

Chapisha