2021
Ni Kwa Nini Unapaswa Kufurahi
Julai 2021


“Ni Kwa Nini Unapaswa Kufurahi,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 6.

Njoo, Unifuate

Ni Kwa Nini Unapaswa Kufurahi

Furahia! Bwana amekupa sababu ya kufanya hivyo.

Mafundisho na Maagano 78:18

Bwana ametupatia mialiko mingi. Na Yeye mara kwa mara anarudia ile iliyo ya muhimu. (Kwa mfano, ni mara ngapi Yeye amesema kitu kama “Njooni kwangu”?)

Moja ya mwaliko unaoupata ukirudiwa katika maandiko ni: “Furahini.”

Bwana nyakati zingine husema hiki pale watu Wake wanapokuwa wanajaribu kumfuata Yeye lakini wanakabiliwa na upinzani na majaribu. Na anapotualika sisi kufurahi, Yeye kwa kawaida hutupatia sababu ya kututia sisi moyo kuwa na furaha hiyo. Kwa mfano, wakati fulani alisema:

“Changamkeni, kwa kuwa nitawaongoza. Ufalme ni wenu na baraka zake ni zenu na utajiri wa milele ni wenu” (Mafundisho na Maagano 78:18).

Hebu tuinyumbue hiyo:

“Changamkeni, kwa kuwa [Sababu ya 1] nitawaongoza. [Sababu ya 2] Ufalme ni wenu [Sababu ya 2a] baraka zake ni zenu, na [Sababu ya 3] utajiri wa milele ni wenu” (Mafundisho na Maagano 78:18).

Hapa Bwana anatukumbusha juu ya mwongozo na baraka Zake. Hizo ni baadhi ya sababu nzuri za kufurahia.

Hapa kuna mfano mwingine.

“Muwe na furaha, watoto wadogo; kwani [Sababu ya 1] Mimi nipo katikati yenu, na [Sababu ya 2] Sijawasahau” (Mafundisho na Maagano 61:36).

Na mwingine.

“Changamkeni, na msiogope, kwani [Sababu ya 1] Mimi Bwana niko pamoja nanyi, na [Sababu ya 2] [MimiI] nitasimama karibu yenu” (Mafundisho na Maagano 68:6).

Bwana anatukumbusha kwamba Yeye yu karibu nasi na atatusaidia tunapojitahidi kumfuata Yeye na kufanya kazi Yake. Tunaweza kisha kwenda zetu kwa kujiamini na, ndiyo, kwa uchangamfu. Kwani, mpango wa Baba wa Mbinguni ni “mpango wa furaha” (Alma 42:8, 16), na kufuata amri za Bwana ni “kuishi kwa furaha” (2 Nefi 5:27).

Hata kama majaribu yetu yanaanza kutulemea, kama tunatamani kumfuata Bwana, Yeye anatuhimiza tufurahie. Na Yeye anatupatia sababu nzuri za kufanya hivyo.

Chapisha