2021
Ufalme wa Selestia unafananaje?
Julai 2021


“Ufalme wa Selestia unafananaje hasa?” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 31.

Kwenye Hoja

Ufalme wa Selestia unafananaje?

Picha
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika ufalme wa selestia.

Utukufu katika Madaraja, na Annie Henrie

Ingawa yawezekana tusiwe na maelezo yote kuhusu ufalme wa selestia, Bwana amefunua baadhi ya kweli kuhusu hilo. Hapa ni baadhi ya mambo tunayoyajua:

  • Kuishi huko inamaanisha kukaa katika uwepo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo tukiwa na mwili mkamilifu uliofufuka na kuishi aina ya maisha ambayo Wao wanaishi. Maisha haya ni “hali ya furaha isiyo na mwisho” (Mosia 2:41) na ni “utimilifu wa shangwe” (3 Nefi 28:10).

  • Wale wanaoishi huko “wamekamilishwa kwa njia ya Yesu,” na “vitu vyote ni mali yao” (Mafundisho na Maagano 76:59, 69).

  • Kuna utukufu mkuu zaidi ya ufalme mwingine wo wote. Utukufu wake umelinganishwa na mng’aro wa jua.

  • Aina hii ya uhusiano tulio nao hapa utakuwepo kule, ikijumuisha uhusiano wa kifamilia, lakini “utazidishiwa utukufu wa milele” (Mafundisho na Maagano 130:2).

  • Unayo madaraja matatu. Daraja la juu zaidi ndipo watu wanaishi wale ambao wameunganishwa pamoja katika ndoa ya milele na wamekuwa wakweli kwenye maagano yao (ona Mafundisho na Maagano 131:1–4).

  • Dunia itapokea utukufu wa selestia (ona Mafundisho na Maagano 88:17–20).

Chapisha