“Maombi kuhusu Miwani ya Kuogelea,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 27.
Misingi Imara
Maombi kuhusu Miwani ya Kuogelea
Wakati mmoja nilienda pamoja na baba yangu huko Sigatoka, Fiji—mahali pazuri sana kuogelea baharini. Wazazi wangu walikuwa wametalikiana, hivyo mama yangu alikuwa haendi pamoja nasi. Kabla hatujaondoka, alininunulia miwani ya kuogelea ya zambarau. Hakika, ni miwani tu, lakini alinitegemea mimi niitunze vizuri na nirudi nayo.
Mwishoni mwa siku ya pili huko Sigatoka, niligundua kwamba sikuwa na miwani yangu. Niliogopa kuwa nisije nikawa nimeipotezea baharini. Kitu cha kwanza nilichokifanya kilikuwa ni kusali ili niweze kuipata miwani yangu. Nilijisikia amani na nilijua kuwa kila kitu kitakuwa SAWA.
Mtu pekee niliyemwambia alikuwa kaka yangu. Yeye haamini katika Mungu na mara kwa mara alipingana na mambo ninayoamini kwa sababu mimi ni muumini peke wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho katika familia yangu. Yeye alisema, “Ndiyo, hutaipata tena.” Nilimwambia, “nimeomba kuhusu hilo, na ninajua maombi yangu yatajibiwa.”
Siku iliyofuata niliangalia vizuri sana majini wakati nikiogelea. Muda wa kuondoka ulipofika, bado nilikuwa sijaipata miwani yangu. Nilikubali pengine nisingeiona tena na nikamshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya faraja na amani.
Kisha kaka yangu ghafla akapiga kelele. Alkuwa amenyanyua miwani ya zambarau.
Kaka yangu bado haamini katika injili, lakini ninashukuru kwa faraja, nguvu, na hakikisho ambavyo vinakuja ninapoweka imani yangu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Shreya S., Suva, Fiji