2021
Shangwe ya Kosei
Julai 2021


“Shangwe ya Kosei,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2021, 12–15.

Shangwe ya Kosei

Kijana huyu kutoka Japani anapenda kushiriki injili na wengine.

Nagasaki, Japani

Picha kutoka Getty Images

Yeye anapiga kinanda. Yeye hukimbia mbio fupi. Pia hupendele michezo ya kuruka! Lakini hayo siyo mambo pekee yanayovutia kuhusu Kosei H., mvulana wa miaka 17 kutoka Nagasaki, Japani.

mvulana akipiga kinanda
mvulana akikimbia

“Yeye ni mmoja wa wamisionari vijana hodari ambaye nimewahi kumjua,” anasema Dada Mckenna Frasure, mmisionari aliyerudi hivi karibuni aliyehudumu huko Japani ambako Kosei anaishi. “Kosei katu hakuacha fursa impite ya kuwa na wamisionari au kushuhudia juu ya Kristo kupitia shughuli za Kanisa na mitandao ya kijamii,” Dada Mckenna anasema.

Kosei anawachukulia wamisionari kuwa ni baadhi ya marafiki zake wa karibu zaidi. Na hii haishangazi kwamba anajisikia hivyo mara unapotambua ni kiasi gani yeye anafurahia kushiriki injili na wengine.

mvulana pamoja na wamisionari

“Kazi ya umisionari ndiyo shangwe yangu,” anasema Kosei. “Nefi alitufundisha kwamba tunda la mti wa uzima ‘ni la kupendeza zaidi ya vitu vyote’ (1 Nefi 11:22). Baadhi ya watu wanaweza kulikataa tunda hili. Hata hivyo, kama mtu anayejua utamu wa tunda hilo, nataka kushiriki injili na wale wanaonizunguka.”

Kushiriki na wengine baraka za injili yaweza kuwa ndio kipaji kikubwa zaidi ya vyote kwa Kosei.

Mafanikio ya Mitandao ya Kijamii

Baada ya kuhudhuria darasa la kujitayarisha kuwa mmisionari, Kosei alihisi hamu kubwa zaidi ya kufikisha shangwe ya injili kwa marafiki zake. Alianza kwa kuingia mtandaoni. Moja ya zana kuu anayotumia ili kushiriki na wengine jumbe za na maudhui ya injili na ni mitandao ya kijamii.

mvulana na simujanja

Baadhi ya marafiki zake wameongelea kile alichokiandika kupitia mitandao ya kijamii. Rafiki mmoja mahsusi alimjia Kosei na kusema, “Mimi napendezwa na kanisa lenu.”

Rafiki huyu alikuwa mtu waliyefahamiana tu hapo mwanzo, lakini urafiki wao kwa haraka ukaota mizizi. “Yeye alianza kwa kuniuliza tofauti kati ya imani yake na yangu,” Kosei anaeleza. “Ingawa sikuwa nimeongea naye mara kwa mara, tulikuja kuwa marafiki wazuri baada ya kushiriki kwangu injili kwenye mtandao wa kijamii.”

Michezo, Mapendeleo, na Urafiki wa Milele

Mitandao ya kijamii siyo njia pekee Kosei anayotumia kushiriki imani yake. Kumbuka, ana maisha ambayo yamejaa shughuli nyingi. Anazo nafasi nyingi za kukutana na watu na kutengeneza marafiki. Na anatumia fursa hizo kusambaza shangwe ya injili.

“Wakati mmoja nilimwalika rafiki wa klabu ya michezo kwenye darasa la Kiingereza ambalo wamisionari walikuwa wakifundisha pale kanisani,” Kosei anaeleza. “Rafiki huyo na wamisionari wakawa marafiki wazuri wakati akijifunza Kiingereza.”

Hata hivyo, maongezi hayakuishia kwenye masomo ya Kiingereza.

“Rafiki yangu alianza kufikiria kuhusu kwa nini wamisionari hawa, ambao walikuwa karibia tu na umri wake, walikuwa wakifanya kazi ya kujitolea na wakihudumu kama wamisionari hapa Japani. Swali lake lililofuata lilikuwa ni kitu gani kinawasukuma wamisionari kuhudumu. Sasa amesikiliza masomo ya wamisionari na bado alikuwa na mawasiliano na wamisionari kwa njia ya kuchati kwa video.”

Wakati wowote Kosei anaposhiriki injili kwa marafiki zake, anajaribu kulinganisha kile anachoshiriki nao na kiwango cha kupendezwa kwao. “Kwa mfano, kwanza ninaongelea kuhusu kile kinachotokea baada ya kifo, nini madhumuni ya maisha haya, au kama Mungu yupo,” yeye anasema. “Kisha naweza kurekebisha, kulingana na mapendeleo yao.”

Ndiyo, yeye anajua kwamba siyo kila mtu atapendezwa. Yeye amekutana na vizuizi, sawa sawa na mtu yeyote. Siku moja, baada ya marafiki zake kadhaa kumwuliza maswali kuhusu Kanisa, Kosei alijaribu kushiriki kipeperushi cha Kanisa na mmoja wao. Hata hivyo, rafiki yule alikimbia nje ya darasa na kutoa kicheko cha nguvu.

“Hiyo ilinisababishia huzuni kubwa,” Kosei anasema.

Lakini haachi kuvunjika moyo kumzuie. Yeye anajua kwamba kitu anachoshiriki nao kitabariki maisha yao milele kama watasikiliza.

Shangwe Inayomsukuma Kutenda

“Ninajisikia shangwe katika mafundisho ya Kristo,” Kosei anasema. “Kama nisingejua mafundisho hayo, ningelikuwa na maisha pasipo shangwe halisi.”

mvulana akisoma maandiko

Wakati anajishughulisha na shughuli zake nyingi na mapendeleo yake mengi, Kosei anajua jinsi ya kuweka vipaumbele. “Injili ya Yesu Kristo inaleta matumaini kwenye maisha yetu na inafunua mambo yote tunayopaswa kufanya,” anasema. “Hata kama tunahisi msongo wa mawazo au tunakuwa na wakati mgumu, maombi ya dhati yataleta amani na kutusaidia kuwa na mtazamo chanya.”

Hiyo ndiyo sababu yeye amedhamiria kushiriki injili kwa kila nafasi anayopata. Yeye anataka na wengine wapate uzoefu wa kile anachokifurahia kila siku! “Ninatumaini kutoka ndani ya moyo wangu kwamba watu wengi waweze kupata fursa ya kuonja shangwe hii halisi,” anasema.

mvulana akiwa hekaluni

Kile Kilicho Muhimu Zaidi

Kwa kawaida, kushiriki injili hakuchukui muda wake wote. Kosei anafanya kazi kwa bidii sana ili kutimiza malengo yake mengine ya maisha. Kila siku anafanya mazoezi magumu ya kukimbia na mazoezi ya kuongeza nguvu. Anapohitaji kujipumzisha kidogo, yeye hupiga kinanda. Yeye pia hufurahia kutembelea sehemu za asilia na kuwa na familia yake. “Nje katika sehemu za asilia na ndugu zangu—sitasahau siku tuliyovua samaki na kuwala!” anasema.

familia
familia inavua samaki
mvulana

Siku zote, hata hivyo, Kosei anaendelea kutenga muda kwa ajili ya kile kilicho cha muhimu zaidi.

Na anao ujumbe mdogo kwa mtu mwingine yeyote anayetaka kufanya vivyo hivyo: “Tunapokea mwongozo tunaposhika amri. Tunapofanya hivyo, tunaweza kuimarishwa na Bwana. Hofu na mashaka mahali pake panachukuliwa na matumaini na kujiamini. Kama tutafungua vinywa vyetu pasipo kuionea aibu injili, watu watakuja kujua upendo kama wa Kristo na watajawa na shangwe.”