2022
Unganika
Januari 2022


“Unganika,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2022, ndani ya jalada la mbele.

Unganika

Viviena K.

17, Tonga

Picha
msichana

Tangu nilipokuwa katika Msingi, nimekuwa nikitamani kuwa mmisionari. Lakini nilipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, nilikatishwa tamaa. Kuwa mkubwa vya kutosha kuhudumu misheni ilionekana ni mbali sana kwangu mimi. Niliogopa kuwa ningeangukia majaribuni. Nilifikiri kuwa ningeliweza kuishi maisha yangu jinsi nilivyotaka na nisijali kuhusu kujitayarisha.

Lakini nilipoongea na wazazi wangu kuhusu kuhudumu misheni, wao walinitia moyo wa kufanya hivyo. Waliniambia Shetani daima atajaribu kunitia majaribuni ninapofanya kitu chema kwa ajili ya Baba yangu wa Mbinguni. Niliomba kwa ajili ya kupata mwongozo, na nilihisi Baba wa Mbinguni akithibitisha kwamba Yeye atakuwa pamoja nami kila siku.

Ingawa nimepitia vishawishi na majaribu, imani yangu ni imara. Ninajua endapo nitajiandaa sasa, kupitia kwa Yesu Kristo, ninaweza kuja kuwa mmisionari kama vile daima nilivyotaka iwe. Yawezekana ikawa vigumu, lakini najua Mungu atakuwa pamoja nami katika kila jambo ninalofanya.

Chapisha