2022
Mwongozo Wetu kwenye Ukweli
Januari 2022


“Mwongozo Wetu kwenye Ukweli,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.

Neno la Mwisho

Mwongozo Wetu kwenye Ukweli

Kutoka kwenye hotuba ya mkutano mkuu wa Oktoba 2004.

mvulana pembeni mwa alama za barabarani

Vielelezo na Emily Davis

Kutoka mahali pako kwenye barabara ya maisha, unazo maili nyingi za kwenda na chaguzi nyingi za kufanya unapotafuta kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni. Pembeni mwa barabara ziko alama nyingi ambazo zinaashiria. Shetani ni mwandishi wa baadhi ya alama hizi. Anatafuta kutukanganya na kutudanganya sisi, ili kutuweka kwenye njia ya chini ambayo inatupeleka mbali na kikomo cha safari yetu ya milele.

mwana mazingaombwe afanya mpira uelee
ramani

Nataka kushirikishi jinsi mnavyoweza kuepuka kudanganywa. Kwanza, ninyi mmefundishwa haki na kuhakikishiwa ukweli wake, hivyo bakini nao. Yashikilieni vyema maandiko, ambayo mafundisho yake hutulinda dhidi ya mwovu. Pili, haitoshi tu kuwa tumepokea ukweli. Ni lazima tumuweke “Roho Mtakatifu awe kiongozi [wetu]” na “siyo [tuwe] walio danganywa” (Mafundisho na Maagano 45:57).

msichana akipokea sakramenti

Tunafanyaje ili Roho Mtakatifu awe kiongozi wetu? Lazima tutubu dhambi zetu na kufanya upya maagano yetu kwa kupokea sakramenti kila wiki tukiwa na mikono na moyo safi. Ni kwa njia hii pekee tunaweza kuwa na ahadi ile ya kiungu kwamba “daima Roho Wake apate kuwa pamoja na [sisi]” (Mafundisho na Maagano 20:77). Roho huyo ndiye Roho Mtakatifu, ambaye kazi yake ni kuwashuhudia Baba na Mwana, kutufundisha sisi, na kutuongoza kwenye ukweli.