“Maswali na Majibu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.
Maswali na Majibu
Sina mambo mengi yanayofanana na watu wa kikundi changu cha vijana. Ninawezaje kuhisi kuunganika nao zaidi?
Kumfikia Yule Mmoja
“Nahisi kuunganika zaidi na wengine ninapojaribu kwa bidii kuutumia muda wangu pamoja na kila mmoja wao, na sio katika mazingira ya kikundi pekee. Kama ukitaka kumpata mtu mnayeendana, mfikie mtu anayeonekana kama anamhitaji rafiki. Yawezekana ukaishia kuwa mwenye kufaidika zaidi kuliko wao!
Latyanna P., umri miaka 17, Singapore
Shiriki Mambo Unayopenda
“Watu wengi katika kikundi changu cha vijana wana vitu tofauti wavipendavyo. Napenda kuwauliza wao kuhusu mambo wayapendayo kwa sababu hiyo inaonyesha kuwa ninawajali. Hii inawapa nafasi wao ya kuniuliza kuhusu mambo niyapendayo pia. Kuunganika na watu huhitaji muda—usichoke!”
Erin F., umri miaka 18, Utah, Marekani
Tafuta Hoja Inayokubaliwa na Wote
“Kama unataka kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na kikundi chako cha marafiki, tafuta mambo mazuri, yenye maana ambayo mnaweza kufanya kwa pamoja, hata kama wao ni wachache. Unaweza kutafuta jambo ulipendalo au la kupitisha muda ambalo nyote mtalifurahia. Omba msaada kutoka kwa Baba wa Mbinguni, na Yeye atakupa mwongozo wa kiungu.”
Carla V., umri miaka 12, Peru
Tambua Vyema Tofauti Zenu
“Kadiri ninavyotumia muda zaidi na watu wa kikundi changu cha vijana, ndivyo ninavyopenda zaidi kitu cha kipekee kuhusu wao! Ninajifunza jinsi ya kuwahudumia vyema, kitu ambacho kinanisaidia mimi kuwa karibu zaidi na wao na kwa Yesu Kristo. Sisi sote ni watoto wa Baba yetu wa Mbinguni, hivyo tunayo mengi yanayofanana kuliko tunavyofikiri.
Sarah M., umri miaka 16, Utah, Marekani
Jaribu Mambo Mapya
“Jitahidi kuwa rafiki na endelea kuongea nao. Endelea kujaribu mambo mapya ili kuwajumuisha wengi zaidi Mvulana mmoja katika kata yetu hakika hapendi michezo, lakini daima anacheza nasi. Kisha tunafanya vitu anavyovipenda, kama vile mitego ya mazingaombwe au kurusha karata. Kujaribu vitu vipya ni njia nzuri ya kuhisi kuunganika.”
Jarren M., umri miaka 17, Nova Scotia, Kanada
Wafikie Wengine
Mfikie na msaidie mtu katika kikundi chako cha vijana ambaye wakati huu anahitaji msaada. Tunapojaribu kuwa mfano wa upendo wa Mwokozi, itatusaidia sisi kuwa wenye kuunganika zaidi kwa kila mmoja.
Joshua C., umri miaka 20, Faleniu, Samoa ya Kiamerika
Kuwa Kile Ulicho
“Kadiri muda unavyopita yawezekana ukayapata mambo mliyonayo yanayofanana, lakini yawezekana siyo papo hapo. Kwa wakati huu, unaweza kuunganika kupitia shughuli ambazo zinafanyika katikati ya wiki. Furahia shughuli! Chagua kushiriki na uwe kile ulicho!”
Hannah W., umri miaka 18, Nova Scotia, Kanada