2022
Kushinda Mbinu za Shetani
Januari 2022


“Kushinda Mbinu za Shetani,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.

Njoo, Unifuate

Musa 14

Kushinda Mbinu za Shetani

Shetani anafanya kila kitu anachoweza ili kutudanganya sisi. Kwa shukrani tunao msaada wa kiungu wa kutuepusha na mitego yake.

mwana mazingaombwe

Mwana mazingaombwe anapiga vidole vyake na mpira unapotea mbele ya macho yako.

Inashangaza!

Kisha anamtoa sungura nje kutoka kwenye kofia ya kichwani iliyo tupu na anafanya kitu kionekane kinaelea.

Wao! Amefanyaje hilo?

Wana mazingaombwe wamegundua jinsi ya kuwafanya watu waamini kuwa wameshuhudia kitu kisichowezekana wakati, katika uhalisia, wao wameona kile tu ambacho mwana mazingaombwe ametaka wao waone.

Hilo ndiyo sahihi! Wana mazingaombwe kiuhalisia hawawaoni wasaidizi wao kuwa nusu. Wamegundua njia za ujanja za kutudanganya sisi katika kufikiria kuwa tumeona kitu ambacho kwa ukweli hakikutokea. Siri ipo katika fikra za uongo na udanganyifu.

Wakati jambo hili lote likifanyika kwa ajili ya kufurahisha na kuburudisha, aina nyingine za fikra za uongo na udanganyifu ni za hatari—kimwili na kiroho.

Fikra za Uongo na Udanganyifu Zilizo Hatarishi

Shetani ni adui wa haki yote na hataki mtu yeyote awafuate Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Yeye anatutaka sisi tuwe na huzuni kama yeye alivyo (ona 2 Nefi 2:27).

Ili kutimiza hili, yeye anafanya kila awezalo ili kutufanya tuwe na shaka au kudharau ukweli wa milele. Anafanya kazi bila kuchoka ili kutuvuruga sisi tuamini kwamba jema ni ovu na ovu ni jema (ona Isaya 5:20). Hii ndiyo sababu yeye nyakati zingine anajulikana kama baba wa uongo na yule mdanganyifu mkubwa (ona Musa 4:4). Na amekuwa akifanya hivi kwa muda mrefu, mrefu sana.

Anguko

Katika Bustani ya Edeni, Mungu aliwaambia Adamu na Hawa wasile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kama wangekula, wangetakiwa kuondoka kutoka kwenye ile Bustani ya Edeni na mwishowe wangekufa. Lakini Mungu aliwaambia kuwa wangeweza kuchagua (ona Musa 3:16–17).

Shetani anataka kuangamiza mpango wa Mungu. Yeye alijaribu kwa kumtamanisha Hawa kula lile tunda lililokatazwa. Alidanganya na kusema kwamba yeye asingekufa (kitu ambacho moja kwa moja kilipingana na kile Mungu alichokuwa amesema). Pia alikuwa amemwambia nusu ya ukweli (ona Musa 4:11).

Mwishowe, Adamu na Hawa walikula lile tunda na wakafukuzwa kutoka katika uwepo wa Mungu. Maandiko yanaita hili kuwa ni “kifo cha kiroho.” Pia wakawa wenye mwili wa kufa, ambayo inamaanisha kwamba wangeweza kufa kimwili. Hii inajulikana kama Anguko.

Kama wazao wa Adamu na Hawa, sisi pia tumetengwa na uwepo wa Mungu na hivyo tutapitia kifo cha kimwili. Pia tunajaribiwa kwa ugumu wa maisha na majaribu ya Shetani.

Hii yote inaweza kusikika kama kitu kibaya, lakini Anguko ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni. Unatupa sisi fursa ya kujifunza na kukua kwa kutumia haki yetu ya kujiamulia ili kuchagua kufanya yaliyo mema. Na kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake, sisi tunaweza kutubu tunapokuwa tumetenda dhambi na kujiandaa kupokea uzima wa milele. Kila kitu ambacho kilitokea kwa sababu ya Anguko, Yesu Kristo anakisahihisha. Shetani hakusimamisha mpango wa Mungu.

Kushinda Mbinu za Shetani

Shetani anaendelea leo kujaribu kutuvuruga na kutudanganya sisi. Hapa kuna njia kadhaa ambazo yeye anatumia kufanya hili:

1. Vishawishi

Shetani anapenda kuweka mawazo machafu na yasiyo ya ukarimu katika njia zetu. Yeye anataka mambo haya yaingie akilini mwetu na ili sisi tuyafanyie kazi. Tunaweza tukakataa vishawishi hivi kwa kumwambia Shetani ondoka (ona ujumbe wa Mzee Stevenson kwenye ukurasa wa 4). Moja ya ulinzi wetu mkubwa dhidi ya vishawishi ni kusali daima (ona Alma 13:28; 3 Nefi 18:15). Tunaweza pia kusoma na kujifunza maandiko. Yanamleta Roho katika mioyo yetu, yanafanya upya hakikisho letu juu ya kile kilicho cha kweli, na kutuwekea ngome imara dhidi ya vishawishi vya siku za usoni.

2. Uongo na Udanganyifu

Shetani nyakati zingine anatuambia vitu kama: “Wewe kamwe hufanyi kitu sahihi,” “Wewe umetenda dhambi sana haiwezekani kusamehewa,” “Haiwezekani kubadilika,” au “Wewe hustahili na hakuna mtu anayejali kuhusu wewe.”

Huu ni uongo. Usiamini! Ukweli ni huu: Mungu anakupenda na anakufurahia wewe kwa sababu wewe ni mtoto Wake. Unastaajabisha! Una uwezekano mkubwa wa kuwa, na kadiri unavyomfuata, siku zako za baadae zinang’ara! Hata unapokuwa umefanya makosa, bado unaweza kuwa na matumaini na, pamoja na Kristo, unaweza kuyageuza mambo.

Unaweza daima kumtegemea Shetani kuwa atakuambia uongo. Unaweza pia daima kutegemea kuwa Roho Mtakatifu atakuambia ukweli (ona Yakobo 4:13). Hiyo ni sababu moja iliyo muhimu ya daima kujitahidi ili Roho awe pamoja nasi.

Tunaweza pia kutambua na kukataa uongo wa Shetani kwa kusoma maandiko kila mara na jumbe za viongozi wa Kanisa. Unaweza kupata maandiko yenye kuinua au nukuu ili zikukumbushe ukweli ambao unapingana na uongo wa Shetani. Unaweza kukariri au kuweka mahali fulani ambapo utaweza kuona mara kwa mara.

3. Kukata Tamaa

Shetani anapenda tunapojihisi kufa moyo. Yeye anataka sisi tuamini kwamba chochote kinachotuvunja moyo kitadumu daima. Lakini hiyo si kweli.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba Shetani anataka sisi tuamini hili kwa sababu “[Shetani] anajua yeye hawezi kuwa bora, yeye hawezi kuendelea, kwamba milele na milele yeye kamwe hatakuwa na kesho angavu. Ni mtu mwenye huzuni kubwa aliyefungwa kwa mipaka ya milele, na anawataka ninyi muwe na huzuni pia. Ndiyo, usiamini hilo.”1

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanakutaka uwe na furaha. Kama tutawageukia, wanaweza kutusaidia kustahimili majaribu na kupata amani na shangwe.

Tunajua Ni Nani Anashinda Mwishowe

Mwokozi anatualika sisi “tumtegemee [Yeye] katika kila wazo; tusitie shaka, tusiogope” (Mafundisho na Maagano 6:36). Tunapotii mwaliko huu, neema na uweza Wake wa kulipia dhambi daima vitakuwa imara zaidi kuliko majaribio ya Shetani ya kutudanganya sisi. Hutupaswi kuangukia kuwa mawindo ya mbinu za Shetani. Tunaweza kuwa na ujasiri na nguvu ili kushinda vishawishi vya Shetani na kuvumilia changamoto za maisha.

Yesu Kristo

Msifadhaike Mioyoni Mwenu, na Howard Lyon

Mwokozi amesema: “Mimi ni nuru ya ulimwengu: yule ambaye ananifuata mimi hatatembea gizani, bali atapata nuru ya uzima” (Yohana 8:12). Yeye pia alisema, “Ulimwenguni mnayo dhiki: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33).

Yesu Kristo anaweza kutuinua juu na kutuimarisha dhidi ya mbinu yoyote ambayo Shetani anajaribu kuitumia dhidi yetu sisi. Kadiri tunavyomkumbuka Mwokozi na mafundisho Yake, tunaweza kuona kupita mbinu za Shetani na fikra zake za uongo na tukaona “vitu kama vile vilivyo” (Yakobo 4:13).