2022
Mtumaini Bwana
Januari 2022


“Mtumaini Bwana,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2022.

Mtumaini Bwana

Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2022

Picha
Mtumaini Bwana
Picha
Mtumaini Bwana

Ulimwengu unavunjika miguuni mwetu.

Anga limejezwa na kijivu.

Mwokozi anawaita kondoo Wake,

Na ataongoza njia.

Tunaijua sauti Yake;

Tumeisikia hapo mwanzo.

Tunajua maneno Asemayo.

Yeye ni nuru.

Tutamfuata Yeye hadi mwisho.

Hata moto ukiunguza

Na dhoruba zikiunguruma,

Giza linapoingia,

Tutaipata Njia yetu ya Kurudi Nyumbani.

Tutamtumaini Bwana.

Hata machozi yakidondoka

Na Marafiki kutuacha,

Sisi twaiona nuru Yake,

Na hapo ndipo tutakapokwenda.

Tutamtumaini Bwana.

Tutamtumaini Bwana.

Hatutapofushwa na mvua;

Njia tuliyomo i wazi.

Milima yaweza kuwa njiani,

Lakini twachagua imani, sio hofu.

Anayafungua macho yetu,

Anatujaza imani,

Anainua nafsi zetu zenye uchovu.

Yeye ni nuru, na kamwe hatuwezi kuwa,

Kamwe hatutakuwa wapweke.

Hata moto ukiunguza

Na dhoruba zikiunguruma,

Giza linapoingia,

Tutaipata Njia ya Kurudi Nyumbani.

Tutamtumaini Bwana.

Hata machozi yakidondoka

Na Marafiki kutuacha,

Sisi twaiona nuru Yake,

Napo ndipo twaenda.

Tutamtumaini Bwana.

Tutamtumaini Bwana.

Kwa mioyo yetu yote,

Tutamtumaini Mmoja tu,

Tutamtumainiya Aliyetuumba.

Hata moto ukiunguza

Na dhoruba zikiunguruma,

Giza linapoingia

Tutaipata Njia ya Kurudi Nyumbani.

Tutamtumaini Bwana.

Hata machozi yakidondoka

Na Marafiki kutuacha,

Sisi twaiona nuru Yake,

Napo ndipo twaenda.

Tutamtumaini Bwana.

Tutamtumaini Bwana.

Tutamtumaini Bwana.

Chapisha