“Ni Vyangu Nami Navijua,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.
Njoo, Unifuate
“Ni Vyangu Nami Navijua”
Je, umewahi kuhisi kuwa wewe si chochote? Yawezekana kuwa umewahi kuhisi hivyo wakati ulipowaza ni watu wangapi wako ulimwenguni au ulipoona wingi wa nyota zilizoko angani. Je, umewahi kujiuliza kama kweli Mungu anakujua wewe ni nani na maisha yako yakoje? Kama ndivyo, basi Musa anao ujumbe kwa ajili yako.
Katika ono, Mungu alimwonyesha Musa kila kipengele cha dunia na watu wote ambao wangeishi humo. Walikuwa “wasiohesabika kama vile mchanga juu ya pwani ya bahari” (Musa 1:28). Mungu kisha akamwambia Musa kwamba ameziumba “dunia zisizo na idadi” (Musa1:33)—kwamba uumbaji Wake umefika nje ya dunia hii.
Musa yawezekana alihisi kulemewa alipoona vitu hivi vyote. Pengine alijiuliza: Mimi naingia wapi miongoni mwa uumbaji huu wote? Na inawezekanaje Mungu kuvikumbuka vitu vingi hivyo?
Jibu la Mungu lilikuwa rahisi tu: “Vitu vyote vinahesabika kwangu” Kivipi? “Ni vyangu nami navijua” (Musa 1:35). Mungu alijua kuwa Musa ni nani, hata kama vile awajuavyo watoto Wake wote, pamoja na uumbaji wake wote. Vyote ni Vyake—nyota, mchanga, na hususani watoto Wake duniani. Wao ndio sababu nzima ya Yeye kuiumba dunia. Wokovu wao wa milele ndiyo kazi muhimu zaidi kwa Mungu.
“Kwa maana tazama, hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).
Kama vile Musa alivyojifunza mahali ambapo yeye anaingia katika mpango wa Mungu, wewe pia unaweza kuhakikishiwa kwamba Mungu anakujua! Kukusaidia wewe kurejea Kwake ni kazi na utukufu Wake. Kwa nini? Kwa sababu wewe ni Wake. Na hakuna kitu ambacho si chochote katika hilo!