2022
Ushawishi wa Rafiki
Januari 2022


“Ushawishi wa Rafiki,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.

Ushawishi wa Rafiki

Miaka ya ujana wangu ilikuwa migumu, lakini Mungu alimtuma rafiki ili anisaidie kuivuka.

wasichana

Kielelezo na Judy Bloomfield

Daima nimekuwa nikijihisi mpweke sana ulimwenguni. Wazazi wangu walitalikiana wakati nikiwa mtoto mchanga, na kisha baada ya miaka michache mama yangu aliolewa tena na tukahamia umbali wa maili 4,000, kutoka Georgia Marekani, kwenda Oregon, Marekani. Yalikuwa mabadiliko makubwa sana kwa msichana wa miaka tisa kuyapata, hususani kwa mwenye lafudhi ya kusini ambaye hakuwa akikubalika kwa watoto wengine.

Nilipoingia shule ya kati, nilikutana na Nicole.* Mara moja, nilihisi hali chanya, ya amani kuhusu yeye—kitu ambacho nilikuwa nakikosa. Nilijua natakiwa kuwa rafiki na msichana huyu!

Kadiri tulivyokuwa tukicheza pamoja zaidi, Nicole alikuja kuwa mahali salama pa upweke wangu. Kuingia nyumbani kwao ilikuwa kama kuingia katika maisha tofauti kabisa: Roho wa Mungu alijaza kila kona. Kulikuwa na picha za Mwokozi na majengo makubwa kila mahali. (Baadae nilijua kuwa haya yalikuwa mahekalu.) Kazi ya umisionari ya Nicole ilianza kwa kunialika tu mimi kwao, na wala hakujua hilo.

Kufanya urafiki na Kuamini

Nicole alinihudumia mimi kwa kuwa tu rafiki yangu. Alinipatia Kitabu cha Mormoni, na tukaanza kusoma pamoja katika gari lake baada ya shule.

wasichana wakiwa na Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni kilianza kujaza mapengo katika maisha yangu. Lakini bado nilijihisi mpweke. Sikuwa mshiriki wa Kanisa la Nicole, lakini pia sikuwa sehemu kamili ya dini ya wazazi wangu.

Nicole kwa ukarimu alinishawishi kuomba na kumwuliza Mungu kama Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Kamwe sikuwa nimewahi kuomba kwa sauti, hivyo sikuwa najua nilipaswa kusema nini. Lakini nilitoka tu nje na kuanza kuongea. Nilimwuliza Mungu kama kanisa la Nicole lilikuwa kanisa sahihi kwangu mimi pia. Punde tu nilipohitimisha swali langu, nilihisi mizizimo kwenye mwili wangu wote. Nilijua, kwa namna fulani pasipo shaka, kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli na Kanisa hili ni sahihi kwangu mimi.

wasichana ndani ya gari

Nilikuwa na umri wa miaka 15 nilipopokea ushahidi huu. Kwa miaka michache iliyofuata niliamini, ingawa wazazi wangu hawakuwa na upendeleo na Kanisa. Lakini sikuwa peke yangu katika imani, kwa sababu Nicole bado alikuwepo akinisaidia.

Imani Mpya, Maswali Mapya

wasichana na wamisionari

Baada ya kumaliza sekondari, nilihamia Utah, Marekani. Nicole tayari alikuwa huko, na alikuwa kwa shauku akisubiria mimi nifike huko ili niweze kuanza kupata masomo ya wamisionari. Nilikuwa na mpango wa kubatizwa kwenye kumbukumbu ya miaka 19 ya kuzaliwa kwangu—wiki sita tu mbele—na Nicole alinihakikishia kuwa angekuwepo pamoja nami wakati wote.

Wamisionari walipoanza kunifundisha, punde niligundua ni kiasi kidogo tu nilikijua kuhusu Kanisa. Nilikuwa nimesoma na nilikipenda Kitabu cha Mormoni, lakini ghafla walikuwa wakiniambia kuhusu kipawa cha Roho Mtakatifu, mpango wa wokovu, kuja kuwa kama Mungu, na mambo mengine mengi mapya. Yalikuwa mengi sana kwa mtu kuweza kufikiria yote kwa wakati mmoja.

wasichana wamekaa kwenye benchi

Lakini Nicole alinijua mimi vizuri. Angeweza kusaidia kuelezea kile wale wamisionari walichokuwa wakinifundisha katika njia ambayo yeye alijua ningeelewa. Katika yale masomo ya kwanza, ufafanuzi wake wa uvumilivu ilikuwa ndiyo sababu niliweza kubakia.

Hatimaye Kuwa Sehemu ya

ubatizo

Nicole kiroho alinisaidia kama hivyo hadi siku nilipobatizwa—na kuendelea. Aliwasaidia washiriki wa kata na wamisionari kupanga ili niweze kubatizwa kwenye kumbukumbu ya miaka 19 ya kuzaliwa kwangu. “Nilipotoka nje ya maji na kuona watu wengi wakinitazama, sikujiona mpweke tena. Kamwe siwezi kusahau hisia ile ya hatimaye kuwa wa Bwana na Kanisa Lake.

Bado ninajifunza kutoka kwa Nicole juu ya uthabiti wa imani na urafiki wake. Alinionyesha kuanzia mwanzo kwamba kazi ya umisionari haihitaji kibandiko chenye jina. Kazi ya umisionari ya Nicole ilianzia ndani ya moyo wake, wakati alipomwendea msichana mwenye lafudhi ya kusini aliyehitaji tabasamu.

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

  • Jina limebadilishwa.