2022
Sehemu ya Burudani
Januari 2022


“Sehemu ya Burudani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2022.

Sehemu ya Burudani

Njia za Kubaki Umeunganika

Kukutana uso kwa uso ni njia kuu ya kuunganika na wengine. Lakini haiwezekani daima kukutana uso kwa uso. Hapa kuna baadhi ya shughuli stahiki za burudani kwa njia ya mtandao zinazofikiriwa mwaka huu kuziba pengo kabla ya kukutana kwenu tena. Shukrani kwa Sarah F. kutoka California, Marekani, kwa kutuma hizi!

  1. Kwa barua pepe tuma kuingo cha ukurasa wa kupaka rangi, toa nakala nyumbani, ipake rangi, na shiriki picha ya ukurasa pamoja na maneno ya kikundi. Kisha andika muhtasari wenye kuburudisha nyuma yake na kisha itume kwa posta kwenda kwa rafiki.

  2. Tengeneza video ya dansi yenye kuburudisha ya sekunde 10 na shiriki na kikundi video hiyo.

  3. Fanyeni shindano la kuweka uso wa kutisha kwa kujipiga picha wenyewe.

  4. Angalieni mawingu angalau siku chache kabla ya kukutana kimtandao. Kila mmoja apige picha ya mawingu ambayo yanaonekana kama kitu fulani, kisha shirikini picha hizo pamoja na waeleze wanafikiri mawingu hayo yanafanana na kitu gani.

  5. Fanyeni mbio za marathoni ya huduma. Oneni ni matendo mangapi ya huduma kila kijana ambaye ni mshiriki wa kikundi anaweza kufanya ndani ya wiki moja na kisha msimuliane mafanikio ya kila mmoja.

  6. Badilishaneni mapishi myapendayo. Onyesha ulichotengeneza kwa njia ya video, na kisha kuleni pamoja.

  7. Fanya mchezo wa kutafuta picha zilizofichwa nyumbani. Andika orodha ya vitu 10 ambavyo unataka vitafutwe nyumbani mwako. Mtu wa kwanza kutuma ujumbe wa picha za vitu vyote 10 anakuwa mshindi!

  8. Fanyeni shindano la vazi kimtandao kwa vitu ambavyo tayari viko nyumbani mwako. Pigeni kura ya iliyo bora zaidi, ya kuchekesha zaidi, ya kipumbavu zaidi, n.k

  9. Fanyeni mbio za kupongezana. Shirikini pongezi nyingi kuhusu kila mmoja kadiri mnavyoweza wakati wa jioni au hata kwa muda mrefu zaidi.

Je, unavyo vitu vingine unavyoweza kuongeza kwenye orodha hii? Vitume kwa ftsoy@ChurchofJesusChrist.org ili tuweze kuvishiriki na vijana wengine.

Mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote

Chora kitu fulani kinachohusiana na dhima ya vijana kwa mwaka huu.

Picha
Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2022

Njia ya kuelekea kwenye Malengo

Je, umejiwekea malengo binafsi ya maendeleo kama sehemu ya Watoto na Vijana kwa mwaka huu? Hapa kuna zoezi dogo lenye kugusa maeneo yote manne ya malengo makuu. Ona kama unaweza kupitia mzingile wote kwa kuzifikia sehemu zote nne za ukaguzi kabla ya kufika katikati!

Picha
msichana

Kielelezo na Josh Talbot

Vichekesho

Picha
baba na mwana

Kuna mtu yeyote aliyeiona raketi yangu ya tenisi?

Val Chadwick Bagley

Jibu la Mzingile

Picha
jibu la mzingile

Chapisha