2022
Jione Mwenyewe kwa Uwazi zaidi
Januari 2022


“Jione Mwenyewe kwa Uwazi Zaidi,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.

Jione Mwenyewe Kwa Uwazi Zaidi

Usiache ulimwengu ukuambie wewe ni nani.

Picha
msichana akijiangalia kwenye dirisha la duka

Ulimwengu utajaribu kukuambia mambo kukuhusu wewe ambayo siyo ya kweli.

“Wewe siyo maarufu vya kutosha.”

Lakini ukweli ni kwamba: urafiki halisi ni wa thamani zaidi kuliko umaarufu.

Picha
mvulana akijiangalia ndani ya kisima cha maji

“Kamwe hautafanikiwa katika kitu chochote.”

Lakini ukweli ni kwamba: imani na bidii ya kazi vinaweza kukufikisha popote unapotaka.

Picha
msichana akijiangalia kwenye kioo

“Wewe ni—” “Ulipaswa kuwa zaidi—” “Hufai—”

Lakini ukweli ni kwamba: Mungu anataka ujione mwenyewe kupitia macho ya kiroho.

Picha
mvulana akijiangalia kwenye kioo cha kutazamia nyuma

“Wewe hustahili!”

Lakini ukweli ni kwamba: wewe ni mtoto wa Mungu.

Picha
mvulana na msichana wanavuta majani na kuona taswira zao katika dimbwi la maji

“Unakosa burudani nyingi sana!”

Lakini ukweli ni kwamba: wewe unapata shangwe unaposhiriki upendo wa Mungu kwa wale wanaokuzunguka.

Picha
mvulana akijiangalia kwenye dira

“Wewe huwezi kufikia chochote!”

Lakini ukweli ni kwamba: siku zako za usoni ni angavu kama imani yako.1

Muhtasari

  1. Ona Thomas S. Monson, “Be of Good Cheer,” mkutano mkuu wa Apr. 2009 (Ensign au Liahona, Mei 2009, 92).

Chapisha