“Je, dunia iliumbwaje?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.
Kwenye Hoja
Je, dunia iliumbwaje?
“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwanzo 1:1). Kwani, alifanyaje hilo? Hapa kuna mambo machache tunayoyajua:
Yesu Kristo aliumba dunia. Baba wa Mbinguni alielekeza kazi ya uumbaji; Yesu Kristo aliitekeleza kwa uweza wa ukuhani. “Kwa njia ya Mwanangu wa Pekee niliumba … dunia” (Musa 2:1).
Ulimwengu uliundwa kutokana na vitu vilivyokuwepo, siyo kutokana na visivyokuwepo. “Tutachukua vifaa hivi, na tutaifanya dunia” (Ibrahimu 3:24).
Uumbaji ulitokea katika hatua sita. Vitu fulani vilitokea katika kila hatua ya Uumbaji. Kwa mfano, mimea ilikuja katika hatua moja, viumbe wa baharini na ndege katika hatua iliyofuata, wanyama na watu katika hatua nyingine.
Hatua hizi za Uumbaji zilichukua kiasi cha muda ambao haukuainishwa. Maandiko wakati mwingine yanaita hatua hizi “siku,” lakini hili si lazima limaanishe siku ya saa 24. Hadithi moja inaelezea juu ya “nyakati” (ona Ibrahimu 4). Sisi hatujui urefu wake.
Maswali yetu kuhusu Uumbaji mwishowe yatajibiwa. “Katika siku ile wakati Bwana atakapokuja, atatufunulia mambo yote—mambo … juu ya dunia hii, ambayo kwayo iliumbwa” (Mafundisho na Maagano 101:32–33).