“Mhandisi wa Shangwe,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2022.
Mhandisi wa Shangwe
Kijana huyu kutoka Ujerumani anapata maarifa, uzuri, na shangwe katika maeneo yote—na anapovipata, anavishiriki na wengine.
Patrick L., umri miaka 16, kutoka Bavaria, Ujerumani, anasema masomo ayapendayo zaidi shuleni ni hisabati, fizikia, na kemia. Ukweli ni kwamba, anaipenda sayansi sana kiasi kwamba alitaka kuwashirikisha wengine kwa kuandika kitabu kuhusu fizikia (juu ya mwendojoto na nguvu za sumaku, ili kuwa sahihi).
Yeye anataka kuwa mhandisi kama kazi yake, akiunda vifaa vya kiufundi kama injini za magari. (Licha ya hayo, makao makuu ya watengeneza magari BMW na Audi yako umbali wa mwendo wa saa moja tu na saa moja na nusu kutoka mahali anapoishi.)
Lakini sayansi si mahali pekee ambapo Patrick anapata vitu vinavyotia nguvu, vinavyomsisimua.
Sayansi na Mawazo ya Ubunifu
Ndiyo, Patrick ana mapenzi ya kina na sayansi, lakini mapenzi yake yanafika mbali zaidi ya baridi, ukweli mgumu, na kanuni.
“Nimeandika kitabu cha fizikia, lakini sasa ninafanya kitabu cha hadithi za kusadikika,” yeye anaeleza. “Kitabu ninachoandika sasa ni kuhusu viumbe wa kimazingaombwe na ulimwengu wao. Na kisha kuna vijana wachache ambao hutoa suluhisho la matatizo hayo.”
Mradi huu wa pembeni ulishawishiwa na mapenzi ya Patrick ya vitabu vya riwaya za kusadikika kama vile Harry Potter na Percy Jackson mwendelezo. Kuandika vitabu kama mradi wa pembeni ni kitu ambacho Patrick amejiingiza baada ya mjomba wake kumwambia inaweza kuwa burudani tosha. “Aliniambukiza shangwe yake hiyo,” anasema Patrick.
Shangwe hiyo yenye kuambukiza imesababisha Patrick kuchukua kile alichojifunza kuhusu kanuni na uhalisia wa ulimwengu na kuandika kitabu kuuhusu. Pia imemfanya atake kuumba hadithi ya kushangaza ya kusadikika. Na hakuna ukinzani katika hili. Patrick anaonekana kujua kwamba ukweli na uzuri na shangwe vinaweza kuonekana sehemu nyingi. Naye anataka kutafuta, kuumba, na kushirikisha wengine vitu hivyo mahali popote wanapoweza kuwa.
Ulimwengu wa Asili
Patrick anaelewa mengi kuhusu sheria za ulimwengu wa asili. Lakini pia huangalia zaidi ya ukweli ili kuona uzuri humo.
“Ninaishi jirani na msitu,” yeye anasema. “Hiyo ni faida ya kuishi katika mji mdogo—unaweza kuingia msituni kwa haraka na kupata amani huko.”
Anapenda njia nyingi za msituni kwa ajili ya wapanda milima, au hasa, waendesha baiskeli. “Napenda kuendesha baiskeli. Ni kitu kikubwa nikipendacho,” anasema. “Naendesha baiskeli mara nyingi. Wakati mmoja niliendesha kilometa 1,200 [745 maili] kwa wiki mbili.”
Wakati mwingine anapenda kwenda kupanda milima au kuendesha baiskeli msituni pamoja na familia nzima (Mama, Baba, kaka zake wadogo wawili, na dada zake wadogo wawili) au na baba yake tu. Mara kwa mara atakwenda peke yake. Lakini daima hupata amani na uzuri katika hali ya asili.
“Kuchomoza kwa jua kunapendeza sana hasa mahali hapa,” anasema. “Wakati mwingine unaweza kuiona milima ya Alps kutokea hapa ingawa iko mbali sana. Na jua linapochomoza, linaonekana kama kwenye kioo, na pamoja na milima, unaona anga zuri jekundu, na hakika inapendeza sana.”
Aina Nyingine ya Maarifa
Kwa nyongeza kwenye sayansi ya asili na uzuri wa ulimwengu wa asili, Patrick pia anathamini ukweli—aina ya ukweli ambao unaweza kuupata tu kupitia sala.
“Ninao ushuhuda imara juu ya sala,” anasema Patrick. “Kupiga magoti chini, kukunja mikono yangu, kuwa na amani na ukimya, na kisha kusali. Hiki ndicho nilicho na ushuhuda nacho.”
Anaelezea kwamba ushuhuda wake unakuja kwa sehemu kutokana na kitu fulani alichoambiwa katika baraka yake ya patriaki. “Inasema kwamba daima napaswa kukumbuka kwamba Baba wa Mbinguni yuko umbali wa sala moja tu kutoka kwangu,” anasema. “Unaweza kuzungumza Naye kila mahali. Yuko hapo kwa ajili yako kila mahali, na unaweza kupata majibu kila mahali.”
Uzoefu wake katika kupokea majibu ya sala unatia moyo, anasema, wakati anapochukua hatua fulani. “Ninahisi Roho Mtakatifu kwa nguvu sana kwa baadhi ya sala. Ninapokuwa makini katika kuweka malengo, ninapokuwa makini kwenye maswali, ninapokuwa makini kwenye kutulia chini na kutenda kama ilivyosemwa katika maandiko na kusubiri na kuwekeza muda—ninapofanikiwa kufanya hivyo, daima ninakuwa na ushuhuda imara na kumhisi Roho Mtakatifu.”
Patrick anakumbuka wakati mmoja alifanya sala maalumu kama hiyo. “Tunazungumza sana kuhusu Joseph Smith na jinsi gani katika umri wa miaka 14 alisali na kupokea jibu,” anasema. “Na hivyo nilikaa chini—na hata nilienda msituni—na nikasali. Nami nikapokea jibu. Kisha nikawa na furaha. Na hiyo ikaimarisha ushuhuda wangu.”
Kushiriki Kile Anachokijua
Kama vile tu alivyotafuta kuwashirikisha wengine maarifa yake ya kisayansi na mawazo yake ya kibunifu, Patrick pia anatafuta kushiriki na wengine maarifa yake ya kiroho.
Kuanzia umri wa miaka 12 ametumia muda wake kuwasaidia wamisionari. Pia wakati mmoja alimwalika rafiki yake nyumbani kwao ili afundishwe na wamisionari. “Tulizungumza kuhusu Urejesho. Alivutiwa sana. Alisikiliza vizuri na kushiriki na kusoma maandiko. Tulisoma Yakobo 1:5, ambayo Joseph Smith pia aliisoma. Na pia nilimfanya asome kutoka katika Joseph Smith—Historia. Hakika alikuwa amejishughulisha.”
Wanafunzi wa darasa lake wanaheshimu imani yake. “Badala ya kulitesa Kanisa, wao walilikubali,” anasema. Hata mwalimu wake katika darasa la dini la shule yake anamuunga mkono. “Anafikiri ni vizuri kuwa nina imani katika Mungu na hata ananisaidia mimi kufikia malengo yangu.”
Baada ya kumaliza shule na kufaulu kwenda masomo ya Chuo kikuu, Patrick pia anapanga kuhudumu misheni. “Pengine nitajiandaa kwa kusoma Preach My Gospel,” anasema. “Ningependa kubaki macho na kusoma, kufanya masomo hayo, na pia kutumia muda mwingi na wamisionari.
Chenye Taarifa Njema
Patrick amejifunza kwamba kuna vitu vingi huko nje ambavyo ni “vyema, vyenye kupendeza, au vyenye taarifa njema au sifa nzuri,” na kwa sababu hiyo anavitafuta vitu hivyo (Makala ya Imani 1:13). Na akivipata, anavishiriki na wengine.
Iwe katika sayansi, mawazo ya ubunifu, au asili, yeye anapata maarifa ya kuvutia na uzuri adhimu popote anapogeukia. Na anapata maarifa ya hali ya juu sana, uzuri, na ukweli kupitia uhusiano wake na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.