Makala
Ushuhuda Wangu
Ninajua kwamba Baba yetu wa Mbinguni anaishi, ninajua kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi na Mkombozi wetu, kuanzia sasa ninajua kwamba familia yangu na mimi tuko katika kanisa la kweli duniani leo.
Nimekuwa muumini wa Kanisa kwa miaka 11, na kwa miaka mitatu ya kwanza nilikuwa nahudhuria Kanisa kama mchunguzi, nimekuwa nikikutana na wamisionari kadhaa ambao walinifundisha. Kila wakati waliponiuliza kuhusu ubatizo, nilirudi nyuma kwa vile familia yangu hawakutaka mimi nijiunge na Kanisa. Mimi binafsi nilisali na kufunga ili Bwana aguse mioyo ya wazazi wangu. Mnamo mwaka 2017 nilimwomba mama yangu kwa upole, kwamba ninapaswa kubatizwa na kwamba yeye pia angeweza kujifunza pamoja na wamisionari.
Ulikuwa uamuzi mgumu sana kwangu mimi kuwakabili wazazi wangu kuhusu Kanisa, lakini baada ya ubatizo wangu Mei 27, 2017, nilipata kuwajua watu walionisaidia kukaa juu ya njia ya agano, licha ya magumu na majanga niliyokabiliana nayo. Hata hivyo, bado nilikuwa na mashaka na familia yangu. Mnamo Juni 3, 2021, niliitwa kumtumikia Bwana katika misioni ya Kinshasa Mashariki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Nilipoingia hekaluni mnamo Juni 12, 2021, kwa ajili ya endaumenti yangu mwenyewe, nilimwomba Baba wa Mbinguni kwa maneno haya,” Baba wa Mbinguni nimekuja kukutumikia Wewe, ombi langu ni kwamba Wewe upate kuwasaidia familia yangu ili kwamba siku moja sisi sote tuweze kuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na tuweze kuingia hekaluni.”
Mama yangu, kaka yangu mkubwa na dada zangu wadogo wote walibatizwa nikiwa katika misheni. Tulikuwa tukiishi na mama kwa miaka 10 pasipo upendo wa baba yangu, na dada zangu na mimi tulikuwa na mama pembeni yetu wakati wote. Nilikuwa na upendo wote kwa baba yangu licha ya ukweli kwamba alikuwa amejitenga nasi kwa miaka 10. Nilipokuwa misheni, nilijua kwamba sipaswi kubadilisha maisha ya wengine wakati familia yangu inaangamia, hivyo, nilifanya kila nilichoweza ili kurudisha mawasiliano na baba yangu.
Nilipowasiliana na baba yangu, nilijua kwamba ninalo jukumu kubwa, kumtambulisha yeye kwa wamisionari. Nilihudhuria mkutano wake wa kwanza na wamisionari kwa njia ya video ya WhatsApp, lakini mara ya kwanza, wamisionari na mimi tulikabiliwa na upinzani na usengenyaji. Baba yangu hakuamini kwamba kunaweza kuwepo na Kanisa la kweli la Mungu ulimwenguni leo. Nilimwomba rais wangu wa misioni kwa ajili ya ruhusa ya upendeleo ya kwenda hekaluni. Nikiwa njiani kwenda hekaluni , nilikuwa nikisali na kufunga kwa ajili ya baba yangu.
Miezi miwili baada ya kurudi kutoka kwenye misheni yangu, Agost 5 na 6, 2023, nilipata heshima ya kumbatiza na kumthibitisha baba yangu na leo sisi sote ni waumini wa Kanisa la yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kupitia sala, kufunga, na tafakuri katika nyumba takatifu ya Bwana. Leo washiriki wote wa familia yangu na mimi tunashiriki Imani ile ile na injili ile ile ya Kristo.
Tunapofuata mfano wa Kristo, tunaweza tukaleta uwezekano wa uongofu wa ulimwengu mzima.