Liahona
Mkenya Mtakatifu wa Siku za Mwisho Mchezaji wa Mpira wa Magongo Mwenye Ndoto ya Kucheza Olimpiki
Machi 2024


Makala

Mkenya Mtakatifu wa Siku za Mwisho Mchezaji wa Mpira wa Magongo Mwenye Ndoto ya Kucheza Olimpiki

Mnamo 2018, Mtakatifu wa Siku za Mwisho Robert Opiyo alijiunga na klabu pekee Afrika Mashariki na Kati ya mpira wa magongo kwenye theluji ijulikanayo kama Kenya Ice Lions. Kwa wakati huo kulikuwa na wachezaji chini ya 30 wa mpira wa magongo kote nchini Kenya, na 17 kati yao (15 wanaume na 2 wanawake) walikuwa wanachama wa timu ya Ice Lions.

Hivi leo kuna zaidi ya wachezaji wakubwa 40 na wachezaji vijana 40 ambao hufanya mazoezi angalau mara mbili kwa wiki. Robert alitumia ujuzi wake aliojifunza katika misheni yake huko Melbourne, Australia, kama mmoja wa wachezaji wakongwe wa timu.

Timu ya Ice Lions ilifanya mazoezi katika barafu ya kutengeneza ya hotelini ambayo ni kubwa mara 2/3 ya barafu inayohitajika katika uwanja wa mpira wa magongo. Mnamo Oktoba 2018, timu ilidhaminiwa kwenda Toronto, Kanada, ili kucheza dhidi ya timu mbili za Kanada zinazoinukia.

Kabla ya mchezo wao wa kwanza huko Toronto, walijifua bila kuwa na mlinda goli. katika mahojiano ya habari huko Toronto, kapteni wa Ice Lions alieleza: “Hatukuwa a vifaa vya golini, na hakuna mtu anayeweza kujihatarisha kuwa kipa bila vifaa stahiki. Hivyo, tulichozoea kukifanya ni kuweka mwanasesere aina ya pengwini na kumweka katikati ya goli na ili kufunga ilibidi kumlenga pengwini juu ya tumbo.”

Kutokana na changamoto za wakati wa UVIKO-19, shughuli za timu zilipoa na kwa sasa zinarejea kawaida. Mara nyingi wanapata msaada kutoka kwa watu binafsi na makundi ambao huchangia fedha kwa ajili ya mazoezi kwenye barafu na kifaa kinachotumika katika mazingira ya kijamii.

Kaka Opiyo ana ndoto ya Olimpiki siku moja lakini pia anaridhika kuwa sehemu ya juhudi hizi za uanzilishi. “Kidogo kidogo watu zaidi husikia kuhusu hamu yetu na kutaka kutusaidia kufika huko,” anasema. “Nina shukrani ya kuwa sehemu ambayo inaweka msingi kwa ajili ya vizazi vijavyo.”