Liahona
Waumini wa Kanisa Wanajiunga katika Juhudi Kubwa ya Kitaifa ili Kupanda Miti Ethiopia
Machi 2024


Makala

Waumini wa Kanisa Wanajiunga katika Juhudi Kubwa ya Kitaifa ili Kupanda Miti Ethiopia

Wakiitikia wito kutoka kwa viongozi wa kiraia, wamisionari na waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho walivumilia hali ya hewa ya mvua mnamo tarehe 15 na 22 Julai 2023 ili kupanda miti huko Addis Ababa, Ethiopia. Rais na Dada Cowley, viongozi wa Misheni ya Addis Ababa Ethiopia, wamisionari wa muda wote na waumini wa Kanisa wenyeji walishiriki katika shughuli hii ya huduma.

Mnamo 2021, Jiji la Addis Ababa liliweka lengo la kupanda miti milioni 25 kwa zaidi ya miaka mitano. Serikali ya taifa inakusudia kupanda mabilioni ya miti kote katika nchi hii kubwa ya Afrika.

Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaamini kwamba wanadamu wote wana usimamizi kwenye dunia na wanapaswa kutumia kwa shukrani kile ambacho Mungu ametoa, kuepuka kutumia ovyo maisha na rasilimali na kutumia viijazavyo dunia kwa ajili ya kuwajali masikini na wenye uhitaji.

Kwenye Mkutano Mkuu wa Oktoba 2022 Askofu msimamizi wa Kanisa, Gérald Caussé, alisema, “Kama watoto wa Mungu, tumepokea agizo la kuwa wasimamizi, walinzi na walezi wa uumbaji Wake mtakatifu.”1

Tanbihi

  1. Bishop Gérald Caussé, “Our Earthly Stewardship”, Liahona, November 2022.

Chapisha