Dondoo za Kitabu cha Maelezo ya Jumla
Muungano wa Usaidizi
9.1 Dhumuni na Mpangilio
Muungano wa Usaidizi huwasaidia watoto wa Mungu kujiandaa kurejea kwenye uwepo Wake. Kama mabinti wa wazazi wa mbinguni, washiriki wa Muungano wa Usaidizi “huelezea maandiko,” “hushawishi kanisa,” huinua mioyo na “hushikilia maagano [ambayo wao] wameyafanya” (Mafundisho na Maagano 25:7, 13).
9.1.1 Dhumuni
Muungano wa Usaidizi ni jumuiya iliyoanzishwa kwa maongozi ya kiungu kwa ajili ya wanawake wote watu wazima ndani ya Kanisa. Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba dhumuni la Muungano wa Usaidizi ni kuokoa nafsi na kupoza taabu. Alisema kwamba Kanisa la Yesu Kristo halikuwa limeanzishwa kikamilifu mpaka akina dada wawe wamepangiliwa.
Washiriki wa Muungano wa Usaidizi hufanya kazi kwa pamoja ili kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Wanawatumikia watu wengine, hutimiza majukumu ya kimaagano, hujenga umoja na kujifunza na kuishi injili.
Kauli mbiu ya Muungano wa Usaidizi ni “Hisani haishindwi kamwe” (1 Wakorintho 13:8). Kauli mbiu hii imewekwa kwenye nembo ya Muungano wa Usaidizi.
9.1.2 Ushiriki katika Muungano wa Usaidizi
Muungano wa Usaidizi ni udada wa maisha yote. Akina dada wote wa miaka 18 na zaidi ni washiriki wa Muungano wa Usaidizi. Ni washiriki hata kama hawawezi kuhudhuria mikutano ya Muungano wa Usaidizi.
Msichana anaweza kuanza kushiriki katika Muungano wa Usaidizi anapofika miaka 18. Anashauriana na wazazi wake na askofu kuhusu muda wa kujiunga. Anapofika miaka 19 au anapoondoka nyumbani, kama vile kwa ajili ya kuhudhuria chuo au kutumikia misheni, anapaswa kuhudhuria katika Muungano wa Usaidizi.
Wanawake walioolewa chini ya miaka 18 pia ni washiriki wa Muungano wa Usaidizi.
9.2 Kushiriki katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa
Mungu huwaalika wote kuja kwa Kristo na kushiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa kwa:
-
Kuishi injili ya Yesu Kristo.
-
Kuwajali wale wenye mahitaji.
-
Kuwaalika wote kupokea injili.
-
Kuunganisha familia kwa milele yote.
Viongozi wa Muungano wa Usaidizi hupanga mikutano ya Jumapili, shughuli, kuhudumiana, huduma na kujumuika kwa aina nyinginezo ili kuwasaidia wanawake kushiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa. Washiriki wa Muungano wa Usaidizi na akidi ya wazee hufanya kazi kwa pamoja ili kukamilisha lengo hili.
Kwa taarifa zaidi kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa, soma sura ya 1.