Liahona
Shangilia katika Zawadi ya Funguo za Ukuhani
Mei 2024


Kikao cha Jumapili Mchana

Shangilia katika Zawadi ya Funguo za Ukuhani

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Bila funguo za ukuhani, hakuna kati yetu ambaye angeweza kufikia ibada muhimu na maagano ambavyo hutuunganisha sisi na wapendwa wetu milele na kuturuhusu hatimaye kuishi na Mungu. …

Funguo za ukuhani hutupatia mamlaka ya kutoa baraka zote zilizoahidiwa kwa Ibrahimu kwa kila mwanamume au mwanamke mshika maagano. Kazi ya Hekaluni hufanya baraka hizi muhimu kupatikana kwa watoto wote wa Mungu, bila kujali wapi au wakati gani waliishi, au wanaishi sasa. …

Funguo za ukuhani zilizorejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith hufanya iwezekane kwa kila mwanamume na mwanamke mshika maagano kufurahia fursa binafsi za thamani za kiroho.

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, hii ni ahadi yangu kwenu. Hakuna kitakachokusaidia ushikilie kwa nguvu zaidi kwenye fimbo ya chuma kuliko kuabudu hekaluni mara nyingi kadiri hali zinavyoruhusu. Hakuna kitakacho kulinda zaidi wakati unapokumbana na ukungu wa giza wa ulimwengui. Hakuna kitakacho imarisha ushuhuda wako juu ya Bwana Yesu Kristo na Upatanisho Wake au kukusaidia uelewe zaidi mpango mtakatifu wa Mungu. Hakuna kitakachoipa faraja zaidi roho yako nyakati za maumivu. Hakuna kitakacho fungua mbingu zaidi. Hakuna!

Hekalu ndilo lango kuelekea baraka kuu zaidi za Mungu alizo nazo kwa ajili ya kila mmoja wetu, kwani hekalu ni sehemu pekee duniani ambapo tunaweza kupokea baraka zote zilizoahidiwa kwa Ibrahimu. …

Acha tufurahie katika urejesho wa funguo za ukuhani, ambazo hufanya iwezekane kwangu na kwako kufurahia kila baraka ya kiroho ambayo tuko tayari na tunastahili kuipokea.

Chapisha