Liahona
Kuunganisha Amri Mbili Kuu
Mei 2024


Kikao cha Jumapili Mchana

Kuunganisha Amri Mbili Kuu

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Acha tuchunguze kila moja ya amri hizi mbili kuu, kama zilivyofunuliwa na kusemwa katika jibu la Mwokozi. Tunapofanya hivyo, ruhusu taswira ya daraja zuri la juu livume katika macho ya akili zako.

Ya kwanza, kumpenda Bwana kwa moyo wako wote, roho na akili.

… Kumpenda Bwana huwa na kiini kwanza kwenye moyo wako—asili yako hasa. Bwana anakutaka kwamba upende kwa roho yako yote—utu wako wote—na mwishowe, upende kwa akili yako yote—mawazo yako na uwezo wako wa kufikiri. … 

… Ninaweza kumpenda Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, ambako kisha huongoza kwenye sala, kujifunza maandiko na kuabudu hekaluni. Tunampenda Baba na Mwana kupitia ulipaji wa zaka, kuitakasa siku ya Sabato, kuishi maisha mema na masafi na kuwa mtiifu.

Kumpenda Bwana huongoza kwenye furaha ya milele!

… Upendo kwa Bwana haukamiliki kama tutawapuuza majirani zetu. Upendo huu wa nje huwajumuisha watoto wote wa Mungu bila kujali jinsia, daraja la kijamii, mbari, kipato, umri au kabila. … 

… Ili daraja lolote la juu liweze kufanya kile lilichokusudiwa kufanya, nguzo zake lazima zifanye kazi pamoja katika upatanifu kamili. Vivyo hivyo, uwezo wetu wa kumfuata Yesu Kristo hutegemea juu ya nguvu na uwezo wetu wa kuishi amri ya kwanza na ya pili kwa usawa na kujitolea kwa dhati kuliko sawa kwenye amri zote mbili. … 

… Na mioyo na akili zetu viinuliwe juu ili kumpenda Bwana na vigeukie upande wa nje, kumpenda jirani yetu.

Chapisha