Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Mvaeni Bwana Yesu Kristo
Dondoo
Baba yetu anataka uhusiano wa kina na wana na mabinti Zake wote, lakini ni uchaguzi wetu. Tunapochagua kumkaribia zaidi Yeye kupitia uhusiano wa agano , inamruhusu Yeye kusogea karibu nasi na kutubariki kikamilifu zaidi.
… Yesu Kristo ni kiini cha maagano yote tunayoyafanya, na baraka za agano zinawezeshwa kwa sababu ya dhabihu Yake ya kulipia dhambi.
Ubatizo kwa kuzamishwa ni lango la kiishara ambalo kupitia hilo tunaingia katika uhusiano wa agano na Mungu. Kuzamishwa ndani ya maji na kutolewa tena ni ishara ya kifo cha Mwokozi na Ufufuko kwa maisha mapya. … Katika Agano Jipya tunasoma, “Maana kama wengi wenu mlivyobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” [Wagalatia 3:27]. …
Ibada ya sakramenti pia inaelekeza kwa Mwokozi. Mkate na maji ni ishara ya mwili na damu ya Kristo iliyomwagwa kwa ajili yetu. … Tunapofanya tendo la kula na kunywa nembo za mwili na damu Yake, Kristo kiishara anakuwa sehemu yetu [ona Yohana 6:56]. …
Tunapofanya maagano na Mungu katika nyumba ya Bwana, tunaongeza zaidi uhusiano wetu na Yeye. Kila kitu tunachofanya hekaluni kinaelekeza kwenye mpango wa Baba yetu kwa ajili yetu, katika kiini chake ni Mwokozi na dhabihu Yake ya kulipia dhambi. …
… Gamenti yetu ya hekaluni inatukumbusha kwamba Mwokozi na baraka za Upatanisho Wake zinatufunika katika maisha yetu yote. Tunapovaa gamenti ya ukuhani mtakatifu kila siku, ishara hiyo nzuri inakuwa sehemu yetu. …
… Ninashuhudia kwamba baraka kuu za uhusiano huo wa agano zina thamani kubwa.