Liahona
Mahekalu, Nyumba za Bwana Zikienea Duniani
Mei 2024


Kikao cha Jumapili Alasiri

Mahekalu, Nyumba za Bwana Zikienea Duniani

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Je, umewahi kujiuliza kwa nini Bwana amemwelekeza nabii Wake sasa kuijaza dunia kwa mahekalu Yake matakatifu? … 

… Sababu moja ni kwamba katikati ya machafuko na majaribu ya ulimwengu, Yeye ameahidi kuwaimarisha na kuwabariki Watakatifu Wake wa agano, na ahadi zake zinatimia! … 

Katika nyumba ya Bwana, kwa uhalisia tunavikwa nguvu za kimbingu. Imani yetu katika Yesu Kristo na upendo wetu kwa ajili Yake vinathibitishwa na kuimarishwa. Tunajifunza kumpenda Yeye hata zaidi. Tunahakikishiwa kiroho juu ya utambulisho wetu wa kweli na madhumuni ya maisha. Tunapokuwa waaminifu, tunabarikiwa na ulinzi dhidi ya majaribu na vivuruga mawazo. Tunausikia upendo wa Mwokozi wetu anapotuinua kutoka katika magumu yetu na changamoto zetu. Tunavikwa silaha ya nguvu za Mungu. …

Wapendwa marafiki zangu, kama tunaweza na kama bado hatujaongeza uhudhuriaji wetu hekaluni, sasa mara kwa mara tutafute muda zaidi wa kuabudu katika nyumba ya Bwana.

Hekalu kiuhalisia ni nyumba ya Bwana. Ninakuahidi wewe unapokuja kwa kustahili na kwa sala kwenye nyumba Yake takatifu, utakuwa umejihami kwa nguvu Zake, jina Lake litakuwa juu yako, malaika Zake watapewa jukumu la kukulinda, nawe utakua katika baraka ya Roho Mtakatifu.

Katika siku hii ya mkanganyiko na vurugu, ninashuhudia kwamba hekalu ni nyumba Yake takatifu, na itasaidia kutuhifadhi, kutulinda na kutuandaa sisi kwa ajili ya siku ile ya utukufu wakati, pamoja na malaika Wake wote watakatifu, Mwokozi wetu atarudi katika enzi, nguvu, na utukufu mkuu.

Chapisha