Liahona
Maagano na Majukumu
Mei 2024


Kikao cha Jumapili Asubuhi

Maagano na Majukumu

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Agano ni ahadi ya kutimiza majukumu fulani. Ahadi binafsi ni muhimu kwa udhibiti wa maisha yetu binafsi na kwa utendaji wa jamii. …

Muda ulipofika kwa ajili ya Urejesho wa utimilifu wa injili ya Yesu Kristo, Mungu alimwita nabii, Joseph Smith. [Kitabu cha Mormoni] ni chanzo kikuu cha Urejesho wa utimilifu wa injili, ikijumuisha mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake, na Kitabu cha Mormoni kimejaa marejeleo ya maagano. …

Maagano yalikuwa jambo la msingi katika Urejesho wa injili. Hili ni dhahiri katika hatua za mwanzo ambapo Bwana alimwelekeza Nabii kulizingatia katika kurejesha Kanisa Lake. …

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linajenga mahekalu ulimwenguni kote. Lengo la mahekalu ni kuwabariki watoto wa agano wa Mungu kwa ibada ya hekaluni na kwa majukumu matakatifu na nguvu na baraka za kipekee za kuunganishwa kwa Kristo wanazozipokea kwa agano.

Kanisa la Yesu Kristo linajulikana kama kanisa ambalo husisitiza kufanya maagano na Mungu. Maagano ni ya kiasili katika kila ibada za wokovu na kuinuliwa ambazo Kanisa hili huzitoa. Ibada ya ubatizo na maagano yake husika ni vigezo vinavyohitajika ili kuingia katika ufalme wa selestia. Ibada na maagano ya hekaluni yanayohusiana nayo ni vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya kuinuliwa katika ufalme wa selestia, ambao ni uzima wa milele, “zawadi iliyo kuu katika zawadi zote za Mungu.”[Mafundisho na Maagano 14:7] Hiyo ndiyo fokasi ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Chapisha