Liahona
Ushuhuda Juu ya Yesu
Mei 2024


Kikao cha Jumapili Mchana

Ushuhuda Juu ya Yesu

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Ushuhuda juu ya Yesu ni nini?

Ni ushahidi wa Roho Mtakatifu kwamba Yeye ni Mwana mtakatifu wa Mungu, Masiya na Mkombozi.

Zaidi ya ushuhuda huu ni swali, Tunafanya nini kuhusu hilo?

Warithi wa ufalme wa selestia “wanapokea” ushuhuda juu ya Yesu katika ufahamu kamili kwa kubatizwa, kumpokea Roho Mtakatifu na kushinda kwa imani. …

Inamaanisha nini kuwa jasiri katika ushuhuda juu ya Yesu?

… Kuwa jasiri katika ushuhuda juu ya Yesu hakika inajumuisha kulea na kuimarisha ushuhuda huo. Wanafunzi wa kweli hawapuuzi mambo yanayoonekana kuwa madogo ambayo yanadumisha na kuimarisha ushuhuda wao juu ya Yesu, kama vile sala, kujifunza maandiko, utii wa Sabato na kula sakramenti, kutubu, uhudumiaji na kuabudu katika nyumba ya Bwana.

Kuwa jasiri pia kunapendekeza kuwa muwazi na kwa watu wote kuhusu ushahidi wa mtu. …

Jambo moja la kuwa jasiri katika ushuhuda juu ya Yesu ni kuwasikiliza wajumbe Wake. …

Kuwa jasiri katika ushuhuda juu ya Yesu kunamaanisha kuwatia moyo wengine, kwa maneno na mfano, wa wewe kuwa jasiri, hasa kwa wale wa familia zetu wenyewe. …

Jambo moja la mwisho la kuwa jasiri katika ushuhuda juu ya Yesu ambalo nitalitaja ni ufuatiliaji wetu binafsi wa utakatifu binafsi. …

Mwaliko wangu ni kutenda sasa ili kupata nafasi yako kama mtu ambaye ni jasiri katika ushuhuda juu ya Yesu.

Chapisha