Liahona
Katika Kuunga Mkono Kizazi Kinachoinukia
Mei 2024


Kikao cha Jumamosi Mchana

Katika Kuunga Mkono Kizazi Kinachoinukia

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Kata nzima itabarikiwa na kuimarishwa kadiri waumini wanavyofokasi kwenye kizazi kinachoinukia. …

Vijana hawa watajifunza mpangilio wa ufunuo wakati wanaposhiriki nasi katika mchakato wa kutafuta na kutenda kulingana na misukumo ya kuwatumikia wengine. Vijana wanapomgeukia Bwana kwa ajili ya mwongozo huu wenye ushawishi wa kiungu, uhusiano wao na tumaini lao Kwake vitaongezeka.

Tunaelezea imani yetu kwa vijana kwa kutoa msaada na mwongozo, bila kuchukua nafasi yao. Tunaporudi nyuma na kuwaruhusu vijana wajifunze kupitia kushauriana pamoja, kuchagua kozi kwa mwongozo wa kiungu, na kuweka mpango wao katika vitendo, watapata furaha na ukuaji wa kweli. …

Vijana wetu wanatushangaza kwa ujasiri wao, imani yao na uwezo wao. Wanapochagua kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo wanaoshiriki kikamilifu, injili Yake itawekwa kwenye mioyo yao. Kumfuata Yeye kutakuwa sehemu ya wao ni nani, siyo tu kile wanachokifanya. …

Vijana leo ni miongoni mwa roho wakuu zaidi wa Baba wa Mbinguni. Walikuwa miongoni mwa watetezi hodari wa ukweli na haki ya kujiamulia katika ulimwengu wa kabla ya kuja duniani. Walizaliwa katika siku hizi kuikusanya Israeli kupitia ushahidi wao wenye nguvu juu ya Bwana Yesu Kristo. Yeye anamjua kila mmoja wao na anajua uwezekano wao mkubwa. Yeye ni mvumilivu kadiri wanavyokua. Yeye atawakomboa na kuwalinda. Yeye atawaponya na kuwaongoza.

Chapisha