Liahona
Kuwa na Umoja pamoja na Kristo
Mei 2024


Kikao cha Jumamosi Mchana

Kuwa na Umoja pamoja na Kristo

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Njoo kwa Kristo, na Casey Childs

Umoja pamoja na Kristo na Baba yetu wa Mbinguni unaweza kupatikana kupitia Upatanisho wa Mwokozi.

Vigezo vya ubatizo, ingawa ni vya maana sana, vina urahisi wa kipekee. Kimsingi vinajumuisha unyenyekevu mbele za Mungu, moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, kutubu dhambi zote, kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo, kuvumilia hadi mwisho, na kuonyesha kwa matendo yetu kwamba tumepokea Roho wa Kristo.

Ni muhimu kwamba vigezo vyote kwa ajili ya ubatizo ni vya kiroho. … Fukara na tajiri wote wanahitajika kuwa na vigezo sawa vya kiroho.

Hakuna utaifa, jinsia au utamaduni vinavyohitajika.

Kwa “mfanano” wetu mbele za Mungu, haileti maana kusisitiza tofauti zetu. …

… Ili kupokea baraka za Upatanisho wa Mwokozi, lazima kwa uthabiti tutumie haki yetu ya kujiamulia kumchagua Kristo na kutii amri Zake.

Chaguzi muhimu zaidi zinaweza kufanywa karibia na kila mtu bila kujali vipaji, uwezo, fursa au hali za kiuchumi. …

Tunapokabiliana na changamoto za maisha, matukio mengi hutokea ambayo kwayo tuna uwezo kidogo juu yake au hatuna udhibiti. Kwa sehemu kubwa ya chaguzi muhimu, tuna uwezo juu yake. …

Kuhusu mambo yahusuyo kanuni, tabia, dini na maisha ya haki, tuna uwezo juu yake. Imani yetu katika na kumwabudu kwetu Mungu Baba na Mwanae, Yesu Kristo, ni uchaguzi ambao tunaufanya. …

Tujitahidi kuwajumuisha wengine kwenye mduara wetu wa umoja. …

Tunaunganishwa kwa upendo wetu juu ya na imani katika Yesu Kristo na kama watoto wa Baba mpendwa wa Mbinguni. Umuhimu wa kuhisi kuwa sehemu ya, ni kuwa na umoja pamoja na Kristo.

Chapisha