Liahona
Shangwe ya Juu Zaidi
Mei 2024


Kikao cha Jumamosi Mchana

Shangwe ya Juu Zaidi

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Cha kusikitisha, inaonekana kwamba, kwa watu wengi, furaha ni ngumu kupata. …

… Kuhisi huzuni sio ishara ya kushindwa. Katika maisha haya, angalau, shangwe na huzuni ni wenza wasiotenganishwa. …

Hata hivyo, pia nimejionea mimi mwenyewe mapambazuko ya utukufu ambayo hujaza nafsi kwa shangwe kubwa sana kiasi kwamba haiwezi kuzuiwa ndani. Nimegundua mwenyewe kwamba ujasiri huu wa amani unatokana na kumfuata Mwokozi na kutembea katika njia Yake.

Amani anayotupa siyo kama ile itolewayo na ulimwengu. “Ni amani bora zaidi. Ni ya juu na takatifu zaidi.

Baba yetu wa Mbinguni hajaificha njia ya furaha. Siyo siri. Inapatikana kwa wote!

Imeahidiwa kwa wale wanaotembea njia ya uanafunzi, kufuata mafundisho na mfano wa Mwokozi, kushika amri Zake na kuheshimu maagano wanayofanya pamoja na Mungu.

Ni asili ya vitu vyote vya kidunia kuzeeka, kuoza, kuchakaa au kuchacha. Lakini shangwe ya Mungu ni ya milele, kwa sababu Mungu ni wa milele.

… Tafadhali niruhusu nipendekeze hatua chache za mwanzo katika safari hii yenye kustahili ya kugundua shangwe safi.

Katika siku zijazo, wiki na miezi, naomba nikualike kwenye:

  • Tumia muda katika juhudi za dhati na za moyoni za kujongea karibu zaidi na Mungu.

  • Tafuta kwa bidii nyakati za kila siku za tumaini, amani na shangwe.

  • Leta shangwe kwa wengine wanaokuzunguka.

Na sote tutafute na kupata shangwe ya juu zaidi ambayo huja kutokana na kuweka wakfu maisha yetu kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe mpendwa.

Chapisha