Liahona
Yote Yatakuwa Sawa Kwa Sababu ya Maagano ya Hekaluni
Mei 2024


Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Yote Yatakuwa Sawa Kwa Sababu ya Maagano ya Hekaluni

Dondoo

Picha
bango

Pakua PDF

Akina Kaka na akina dada, ninashuhudia kwa unyenyekevu kwamba tunapohudhuria hekaluni, tunaweza kukumbushwa asili ya milele ya roho zetu, uhusiano wetu na Baba na Mwanawe mtakatifu, na tamanio letu la mwisho la kurudi nyumbani kwetu mbinguni. …

Chini ya uongozi wenye mwongozo wa kiungu wa Rais Nelson, Bwana ameharakisha, na ataendelea kuharakisha, ujenzi wa mahekalu kote ulimwenguni. Hii itawapa watoto wote wa Mungu fursa ya kupokea ibada za wokovu na kuinuliwa na kufanya na kushika maagano matakatifu.

Ushiriki wa kila mara katika ibada za hekaluni unaweza kujenga mpangilio wa msimamo kwa Bwana. Unaposhika maagano yako ya hekaluni na kuyakumbuka, unaalika wenza wa Roho Mtakatifu ili kukuimarisha na kukutakasa.

Ni kupitia maagano ya kuunganishwa katika hekalu kwamba tunaweza kupokea hakikisho la miunganiko ya upendo ya familia ambayo itaendelea baada ya kifo na kudumu milele. Kuheshimu maagano ya ndoa na familia yaliyofanywa katika mahekalu ya Mungu kutatupatia ulinzi dhidi ya uovu wa ubinafsi na kiburi. …

Majaribu, changamoto, na machungu hakika yatakuja kwetu sote. Hakuna yeyote kati yetu aliye na kinga dhidi ya “miiba ya mwili” [ona 2 Wakorintho 12:7–10]. Hata hivyo, tunapohudhuria hekaluni na kukumbuka maagano yetu, tunaweza kujiandaa kupokea maelekezo binafsi kutoka kwa Bwana.

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, ninatoa ushahidi kwamba hakuna chochote kilicho muhimu zaidi ya kuyaheshimu maagano uliyoyafanya au unayoweza kuyafanya hekaluni.

Chapisha