2021
Mzee Cook Anazuru Ufilipino
Mei/Juni 2021


Mitume kote Ulimwenguni

Mzee Cook Anazuru Ufilipino

Mitume wanawahudumia watu kote ulimwenguni na kuwafundisha kuhusu Yesu Kristo.

Picha
Elder Cook speaking to members

Wakati Mzee Quentin L. Cook na Dada Mary Cook wakiwa Ufilipino, volkano kubwa ililipuka. Walifurahi kuwa walikuwa huko kusaidia na kuwafariji watu.

Picha
family sleeping in Church building

Hewa ilijaa majivu kiasi kwamba ilikuwa vigumu kupumua. Watu walilazimika kuacha nyumba zao. Familia nyingi walilala katika majengo ya Kanisa.

Picha
Elder Cook speaking to child

Mzee Cook aliwaambia watu kuwa Baba wa Mbinguni anawapenda na kwamba angewasaidia.

Picha
Elder Cook thanking people

Mzee Cook aliwashukuru waumini wa Kanisa kwa huduma yao kama ya Kristo kwa kila mmoja wao na kwa marafiki wa imani zingine.

* Imechukuliwa kutoka Church News, Jan. 14, 2020.

Chapisha