2021
Nilipiga Wimbo wa Kanisa
Mei/Juni 2021


Imeandikwa na Wewe

Nilipiga Wimbo wa Kanisa!

Picha
boy playing piano

Kwa mara ya kwanza niliposikia kaka yangu mkubwa akipiga kinanda katika mkutano wa sakramenti, nami nilitamani kufanya vivyo hivyo. Lilikuja kuwa lengo langu la programu ya Watoto na Vijana kupiga wimbo wa kanisa katika mkutano wa sakramenti.

Tangu hapo, nimekuwa nikijifunza kinanda pamoja na mjomba wangu Ken. Kila siku najaribu kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30. Baada ya miezi 10, niliweza kupiga wimbo wa “Sala ya Kwanza ya Joseph Smith” (Wimbo wa Kanisa, na. 26).

Kisha ikaja COVID-19. Viongozi wa Kanisa wakafuta mikutano ya Jumapili. Walisema tunapaswa kuwa na kanisa nyumbani. Mama na Baba walitupangia kila mmoja kazi. Waliniomba nipige wimbo wa kufungua, nami nikapiga “Sala ya Kwanza ya Joseph Smith.” Niliweza kutimiza lengo langu la kupiga wimbo wa kanisa katika mkutano wa sakramenti! Niliweza kuhisi Roho katika nyumba yetu.

Chapisha